Na Mwandishi Wetu,TimesMajira Online Dodoma
GARI la kwanza katika Kampeni ya Bonge la Mpango inayoendeshwa na Benki ya NMB, leo ilikabidhiwa kwa, Hadija Iddi mkazi wa Chamwino, mkoani Dodoma.
Hadija anakuwa mshindi wa kwanza katika zawadi kubwa zinazotolewa na Benki ya NMB katika Kampeni iliyoanza Februari, mwaka huu ambapo alikabidhiwa gari hiyo aina ya Tata Ace (Kirikuu) lenye thamani ya sh. milioni 25.
Akizungumza leo jijini Dodoma, Kaimu Afisa Mkuu Ukaguzi wa Ndani wa NMB, Benedicto Baragomwa amesema kampeni hiyo inayoelendea nchini nzima ina zawadi mbalimbali ambazo zinaendelea kutolewa.
Baragomwa amesema NMB inatoa zawadi kwa wateja wanaoendelea kufungua akaunti zao na kuwa mshindi wa jumla atajinyakulia gari ya Toyota Fortuner yenye thamani ya sh. milioni 169.
“Ndugu Watanzania, hapa namkabidhi Hadija ufunguo wa gari yake kama mnavyoona ni jipya, lakini tunazo zawadi nyingi kwa wateja wetu wanaoweka akiba kuanzia sh. 100,000 kwenye akaunti zao za NMB,” amesema Baragomwa.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa gari yake, Hadija amesema hajaamini kilichotokea na kuwa hakuwa amepanga, lakini ni mpango wa Mungu.
Hadija amesema gari hiyo TATA Ace yenye thamani ya sh. milioni 25 itamsaidia katika shughuli zake za kujiongezea kipato na kuwashauri Watanzania kuwekeza katika huduma za benki kwa kuwa ina manufaa makubwa.
“Nimeamini kuwa yanayozungumzwa ni kweli,nimekabidhiwa gari mpya,nimepewa ufunguo na kadi ya gari vikiwa kamili kabisa, kweli NMB ndiyo mpango mzima,”amesema Hadija.
Wakati huo huo Meneja wa NMB kanda ya Kati Nsolo Mulozi aliongoza droo nyingine kwa ajili ya ya washindi ambapo watu mbalimbali walipata fedha baada ya kushinda.
Droo hiyo imifanyikia katika Tawi la NMB Chamwino Ikulu chini ya usimamizi wa viongozi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha.
Amesema hadi sasa zawadi zenye thamani ya zaidi ya sh. milioni 145 zikiwemo fedha taslimu, pikipiki za miguu mitatu aina ya LIFAN 16 na gari tayari zimakwisha tolewa na NMB.
More Stories
Rais Samia afurahia usimamizi mzuri wa miradi
Rais Samia apongezwa kwa kuboresha huduma kwa wazee
Watu 5,000 kuhudhuria tamasha la utamaduni Songea