Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala
Mwanafunzi wa Kidato cha nne shule ya Benjamini Mkapa Angela Tumsifu Minja, (18) amepata fursa ya kuteuliwa kushiriki mashindano ya Basketi ball nchini Marekani.
Akizungumza na waandishi wa habari Wilayani Ilala leo Mkuu wa Benjamini Mkapa Joseph Deo, alisema mwanafunzi Angela ni miongoni mwa mwa wanafunzi saba walioshiriki mashindano ya Umoja wa Shule za Sekondari (UMISSETA) Taifa na kufanya vizuri fainali hizo akitokea mkoa Dar es Salaam shule ya Benjamini sasa hivi anaelekea Marekani katika michezo ya Basketi ball.
“Mwanafunzi wetu Angela Tumsifu Minja, anaenda Marekani katika michezo ya Basketi ball ,tunampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, kukuza sekta michezo katika nchi yetu tumeweza kuitangaza Tanzania kupitia michezo “alisema Deo
Akielezea mafanikio ya shule ya Sekondari Benjamini Mkapa kitaaluma sekta michezo alisema shule ya Benjamini Mkapa imefanikiwa kuleta vikombe vya mashidano ya CAF na CECAFA katika mashindano ya Afrika Mashariki kwa shule za Sekondari ambapo shule hiyo inashiriki kila mwaka ,vikombe vingine vya usafi na Mazingira kila mwaka Benjamini Mkapa inakuwa ya kwanza.
Alisema Mwanafunzi Angela Tumsifu akimaliza masomo yake mwaka huu atapata udhamini wa Masomo nchini Marekani huku akiwa mwanamichezo wa Basketi ball kutokea Tanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari Mwanafunzi Angela Tumsifu (18) aliwashukuru Walimu wa shule ya Benjamini na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Mkuu wa Wilaya ya Ilala na makocha wa Vijana klabu .
Mwanafunzi Angela alisema safari yake ya Marekani anaondoka Julai 11na Ndege katika kambi ya siku saba Marekani.
Angela alisema akimaliza elimu yake ya sekondari atajiendeleza na kutangaza nchi yake akiwa Marekani.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa