January 11, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mwanafunzi aungua moto wakati akipika maharage

Na Thomas Kiani,TimesMajira,Ikungi

MWANAFUNZI wa darasa la tano katika shule ya msingi Msugua iliyopo katika kijiji cha Msugua kata ya Sepuka Wilaya ya Ikungi mkoani Singida Kuruthumu Yoel (13) ameungua moto katika sehemu mbalimbali za mwili wake wakati akipika nyumbani kwao.

Akizungumza na Majira bibi wa mtoto huyo Neema Kibulii amesema kuwa
Tukio hilo limetokea juzi saa 4 asubuhi wakati mwanafunzi huyo akiwa na mwanfunzi mwenzake wa darasa la wakipika mboga aina ya maharage.

Amesema kuwa watoto hao walikuwa jikoni wakipika na wamemueleza kuwa walikuwa wakichochea kuni na mmojawapo alikanyaga kipande wa kuni ambacho kilirukia kwenye nguo za Kuruthum na kusambazaa mwilini.

Kwa habari zaidi soma kesho Gazeti la Majira