Na Mwandishi wetu -Mpwapwa.
Mtandao wa Marafiki Elimu wilayani Mpwapwa chini ya uratibu wa Shirika la HAKIELIMU umebaini ongezeko la uwandikishaji wa watoto wenye mahitaji maluum katika shule za Msingi kwa miaka mitatu 2022- 2024 japo kuwa kuna uhaba wa walimu wenye ujuzi wa kufundisha Elimu jumuishi ni mkubwa.
Akifungua kikao cha uwasilishwaji wa ropoti ya ufuatiliaji mkakati wa taifa wa Elimu jumuishi wa mwaka 2022 Hadi mwaka 2026 Kaimu Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa,Obert Mwalyego amesema ongezeko hilo limesababishwa na na uwapo wa Miundo Mbinu rafiki Kwa shule za Msingi na sekondari.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtandao wa Marafiki Elimu wilaya ya Mpwapwa, Stephen Lwitiko amesema katika shule 20 zilizotembeleaa zilikuwa na walimu 212 lakini wenye ujuzi wa kufundisha Elimu jumuishi walikuwa walimu Kumi na mmoja tu.
Pia Lwitiko amedai kuwa muongozo wa serikali utoa kuanzia kiasi cha shilingi 26,000 Kwa mtoto mmoja Kwa mwezi Kwa ajili ya chakula lakini kulikuwa na utofauti wa upokeaji wa viwango vya fedha kuanzia shilingi elfukumi na Tano (15000)Hadi elfu ishirini na sita na mia nne(26’400) Kwa mtoto mmoja Kwa mwezi.
Mmoja wa shiriki wa mkutano huo bwana Kandido Mnemele amesema yeye pamoja na ulemavu wake lakini alihamasishwa na mwalimu kuanza shule kitu alichokisema kuwa Walimu wananafasi kubwa Kwa kuhakikisha walemavu wanapata Elimu kama ilivyo Haki ya Msingi Kwa wote
Hata hivyo Mwakilishi wa Shirika la HakiElimu,Naomi mwakilembe amesema marafikielimu wamezifikia shule 20 kati 139 za wilaya ya Mpwapwa hivyo wanatakiwa kuunganisha nguvu Ili shule zote zinafikiwa na watoto wote wenye ulemavu wanapata Elimu.
More Stories
Polisi yaonya vyama vya siasa
Mzumbe yaanika siri ya shahada udaktari wa heshima kwa Samia
Kujenga ofisi ya kisasa,akipewa ridhaa ya Uenyekiti