December 27, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mwalimu asiyeona asimulia alivyoachwa na Mume wake

Na Esther Macha, Timesmajira, Online, Mbeya

JAMII imeaswa kuacha mila potofu ya kuwatenga na kuwanyanyapaa watu wanaopata matatizo ambayo usababisha ulemavu wa kudumu na badala yake wawe mstari wa mbele kuwasaidia katika mahitaji mbalimbali .

Akizungumza na Timesmajira leo jijini Mbeya ,Mwalimu wa shule ya msingi mchanganyiko ya Katumba 2 , Happy Mwampiki ambaye ana changamoto ya kutoona amesema hayo wakati wa mafunzo ya kujengewa uwezo kwa baadhi walimu wanaofundisha shule za watoto wenye ulemavu yaliyoandaliwa na taasisi isiyo ya kiserikali ya Child support Tanzania (CST) iliyopo Jijini Mbeya.

Happy ambaye ni mwalimu asiyeoona ambaye alipata tatizo hilo akiwa ndani ya ndoa yake jambo ambalo lilipelekea kuachwa na mwenza wake kwa sababu ya ulemavu alioupata.

Akielezea zaidi Happy amesema kuwa mume wake alipomuacha alifika Ofisi za Ofisa Elimu mkoa wa Mbeya kuomba nafasi ya kufundisha watoto wenye ulemavu alifanikiwa kupata ajira katika shule ya msingi mchanganyiko ya Katumba iliyopo Wilayani Rungwe.

“Nilianza kazi ya kufundisha watoto wasioona katika shule ya Katumba ambapo sasa nipo hapo, lakini nikiwa shuleni hapo nikiendelea na kazi walimu wasioona niliowakuta shuleni hapo walijaribu kunifundisha jinsi ya kufundisha watoto wasioona nikaweza na naendelea na kazi hiyo mpaka Sasa “amesema Mwalimu Happy.

Aidha Mwalimu Happy amesema kuwa akiwa shuleni hapo hakukata tamaa kuhangaikia tiba ya macho yake ikiwemo Hospitali ya Muhimbili, Mvumi, pamoja na Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya na kuambiwa kuwa ana makovu kwenye Letina ya jicho.

Happy amesema kuwa mara baada ya kupata ajira aliomba kwa uchungu na machozi kwa Mungu ili Mume wake aliyemuacha apate kazi hivyo alifanikiwa kupata uteuzi mkubwa katika mambo ya Sayansi na Teknolojia na kuwa Mkurugenzi.

Akifafanua zaidi Happy amesema kuwa ndugu zake na jamii walisema mume wake kamloga kwasababu ana fedha nyingi lakini haikutosha bado jamii walidai amerogwa na wazazi lakini hakuwahi kukubali kwasababu anawajua wazazi wake kuwa hawezi kuwasemea habari zao haamini ushirkina kwa wazazi wake na kuwa tatizo lake ni mambo ya kibalojia tu.

Akizungumza na Timesmajira Meneja miradi wa Child support Tanzania, Hildergade Mehrab amesema kuwa katika kuhakikisha elimu ya ulinzi Jumuishi inafika taasisi hiyo imetoa mafunzo ya siku ya tatu ya kuwajengea uwezo walimu ambapo kila shule ilichukua walimu wanne wakiwemo mwalimu Mkuu na walimu watatu kwa ajili ya kuwajengea uwezo wa kutetea haki za binadamu hususani watoto wenye ulemavu.