January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mwakinyo kuzichapa na Kiduku

Na Iddy Lugendo, Timesmajira Online DSM

BONDIA Hassan Mwakinyo baada ya kumpiga Bondia wa Ghana Elvis kwa KO katika raundi ya 7 kwa mara nyingine ametuma salamu Morogoro (Kwa Twaha Kiduku) akisema hamuogopi na kama atatokea Promota wa kuweka dau kubwa yupo tayari kupigana nae hata pambano la kirafiki ili ajulikane nani ni Mbabe kati yao.

Mwakinyo alisema “Elvis sio Bondia rahisi na hajawahi kupoteza kwa KO hii ni ya mara yake ya kwanza na ni Bondia ambaye anacheza kilo 78 Mimi nimempandia uzito ni kiu changu cha muda mrefu lakini nilitaka kuwaprove WBO kwamba mwili wangu na uwezo nilionao ni vitu tofauti”

“Lakini pia nilikuwa nataka kutuma salamu Morogoro kwa Watu ambao walikuwa wanaamini naogopa zile piko kama Mabibi harusi wa huku , nilikuwa nataka kutumia hii fursa kama mfano wa kuonesha kwamba dau likifikwa ambalo lipo katika makubaliano yangu Mimi na Timu yangu pambano litapigwa hata la kirafiki ili tuone nani ni nani!?”

Pia Hassan Mwakinyo baada ya kumpiga Bondia wa Ghana Elvis kwa KO katika raundi ya 7 amewashukuru Waandaaji wa pambano hilo kwa kumpa fursa ya kuwaonesha Mashabiki kuwa yeye ni Mpiganaji wa aina huku akisema anaamini kufa kwa Imam sio mwisho wa kufanya Ibada hivyo hata wakati ambao alikuwa hapati nafasi haikumvunja moyo.

Mwakinyo amenukuliwa akisema “Namshukuru Mungu pia Waandaaji wa pambano kwa kunipa nafasi ya kuonesha Mashabiki zangu kuwa Mimi ni Mpiganaji wa aina gani, mara zote nimekuwa nikiamini kwamba kufa kwa Imam sio mwisho wa kufanya Ibada, akifa Imam inabidi utafute Imam mwingine Ibada ziendelee”

“Hata wakati ambao nilikuwa sipati nafasi ilikuwa hainivunji moyo nilikuwa naamini ipo siku nitapata nafasi ambayo inastahili sawa na heshima yangu, nawashukuru Mashabiki zangu kwakuwa wamenivumilia muda mrefu wameonesha nguvu kubwa ya kufuatilia pambano langu lakini pia namshukuru Mungu ameniwezesha kufanya ambacho nilikuwa nastahili kufanya kwa muda mrefu kwao” alisema

Bondia Hassan Mwakinyo ameshinda pambano hilo Januari 28, 2024 kwa kumpiga Bondia wa Ghana Elvis kwa KO katika round ya 7 ya pambano hilo la kuwania ubingwa wa WBO Africa ambalo limepigwa New Amaan Complex Zanzibar.