Na Martha Fatael, Moshi
MAMLAKA ya Maji safi na usafi wa mazingira Moshi (Muwsa), imeanza Utekelezaji wa agizo la kufunga Mita za malipo kabla ya matumizi (Prepaid meters) Rais la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu alitoa kwa Wizara ya Maji kuanza matumizi ya teknolojia ya mita hizo kwa wateja ili kuboresha huduma na kupunguza changamoto za ankara kwa Wananchi.
Zaidi ya Mita 460 tayari zimefungwa katika makazi na ofisi za Jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro ambao walikuwa na deni la zaidi ya Sh Bil 2 ambalo linaendelea kulipwa kwa awamu.
Taarifa hiyo inatolewa na Kaimu mkurugenzi wa Muwsa, Edes Mushi ambaye anasema lengo kubwa la ufungaji wa mita hizo ni kukabiliana na changamoto mbalimbali kati yao na wateja, zikiwemo za madeni sugu, madai ya kutopewa bili sahihi na mengine ya usomaji mita.
Amesema kati ya wateja ambao ni wadaiwa sugu ni jeshi la polisi ambalo tayari Jeshi hilo limelipa sehemu ya deni hilo na sasa wanadaiwa takribani Sh Bil 1.7 deni ambao lipo kwenye makubaliana ya malipo endelevu.
“Tukiwa tunasherehekea wiki ya maji taarifa tuliyonayo muhimu ni kuwa kwa sasatumeweka nguvu katika kuhakikisha tunatoa huduma kwa saa 24 ili kuendelea kuongeza ubora wa huduma zetu”Anasema Mushi

Mushi amesema huduma ya mita hizo itaendelea kufungwa kwenye taasisi nyingine kama Jeshi la magereza na baada ya kukamilika kwake ndio zitahamia kwa wateja wake wa nyumbani na ofisi binafsi.
Amesema gharama za ufungaji wa mita hizo ni kubwa hivyo kwa sasa wanaendelea na mchakato wa utafutaji raslimali fedha kwani Mita za Prepaid moja ni wastani wa Sh 400,000 Hadi 600,000 huku zile za kawaida ni kati ya Sh 100,000 hadi 120,000 gharama ambazo hapaswi kutozwa mteja.
Aidha Mushi amesema pamoja na mafanikio hayo mamlaka hiyo inakabiliwa na changamoto mbili kubwa ikiwemo ya upotevu wa maji na baadhi ya wananchi kukataa kufungiwa mita hivyo kuzua migogoro.
“Hii changamoto ya kukataa kufungiiwa mita tunapambana nayo kwa mujibu wa sheria lakini pia kwa kutoa elimu maana wateja wa maeneo ya pembezoni wanakataa kufungiwa Mita kwa madai maji ni mali ya Mungu…… baadhi ya Mita ziling’olewa na kutekelezwa vichakani katika sehemu ya kata 12 ambazo ni maeneo pembezoni” amesema

Kuhusu upotevu wa maji, Mushi amesema mamlaka ya udhibiti wa Nishati na maji (Ewura) inazitaka mamlaka kuwa chini ya asilimia 20 changamoto ambayo mamlaka hiyo inaweka nguvu kuifanyia kazi kwani kwa sasa mamlaka hiyo ina upotevu wa asilimia 22 ikilinganishwa na kiwango kilichowekwa.
Awali wakiongelea maadhimisho ya wiki ya maji, baadhi ya wakazi wa Moshi Rita Sumari, Liberatus Massawe wameiomba MUWSA kutizamwa upya kwa mamlaka ya wasomaji wa mita kwani hawatumii lugha nzuri kuelimisha wateja kuhusu usomaji mita wao.
“Binafsi nashukuru huduma ya maji safi na majitaka zote Napata vizuri….tatizo langu ni pale ambako sielewi bili yangu nikiuliza wasoma mita wananijibu vibaya na huwa wanajiona wao ni wa mwisho….utake usitake utalipa hiyo bili….hii sio sawa”anasema Massawe
More Stories
Kakulima:Lushoto ni eneo muhimu kwa shughuli za utalii
Viongozi CHADEMA, Odinga wakutana, wajadili hali ya kisiasa nchini
Kamati ya Bunge yaridhishwa na ujenzi wa miradi kupitia mapato ya ndani