Na Allan Vicent, TimesMajira Online Tabora
MUUGUZI wa Hospitali ya Wilaya ya Sikonge Mkoani Tabora Rayson Duwe anayetuhumiwa kubaka mama mjamzito majira ya usiku hospitalini hapo imeendelea kuunguruma katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Sikonge.
Hukumu ya kesi hiyo inatarajiwa kutolewa tarehe 15 mwezi ujao mahakamani hapo baada ya mashahidi wa pande zote mbili kukamilisha utetezi wao.
Mtuhumiwa huyo ambaye ni Muuguzi Msaidizi daraja la pili alitenda kosa hilo mwezi Juni mwaka huu akiwa zamu usiku alipokuwa akimhudumia ambapo alimchoma sindano yenye dawa ya usingizi na kumfanyia kitendo hicho.
Mama huyo alifanyiwa kitendo hicho akiwa na ujauzito wa miezi 9 na mtuhumiwa alikutwa na watumishi wenzake akiwa pembeni ya kitanda alicholazwa mama huyo aliyekuwa akisumbuliwa na homa, mtuhumiwa yuko nje kwa dhamana.
Wakati huo huo Mahakama hiyo imemhukumu kifungo cha maisha jela Ngasa Polepole (19) mkazi wa Kijiji cha Madole tisa baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kulawiti mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 4.
Hakimu wa Mahakama hiyo Irene Lyatuu alisema siku ya tukio mtuhumiwa alimchukua mtoto huyo akiwa na wenzake na kuwapeleka porini kwenda kutafuta matunda pori ndipo alipomfanyia kitendo hicho akiwa na wenzake.
Akitoa hukumu hiyo Hakimu Irene alisema mahakama imejiridhisha pasipo shaka kuwa mtuhumiwa alihusika moja kwa moja kutenda kosa hilo la udhalilishaji watoto kinyume na sheria.
More Stories
‘Ni Wasira ‘Makamu Mwenyekiti CCM Bara
15 mbaroni tuhuma wizi wa shehena ya unga wa sembe
Wacheza rafu Uchaguzi Mkuu ujao waonywa