Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Ziwa Joseph Mutalemwa amewasihi wakazi wa Bariadi na nchi nzima kuendelea kutumia huduma mbalimbali za mtandao huo mara kwa mara ili kujiongezea nafasi ya kushinda zawadi.
Mutalemwa ameyasema hayo leo wakati akikabidhi kiasi cha Shilingi Milioni Tano kwa Robin Brasio ambaye ni mkazi wa eneo la Kidinda na miliki wa duka la spea za pikipiki wilayani Bariadi mkoani Simiyu, baada ya kuibuka mshindi kwenye promosheni ya Magifti Dabodabo.
“Mtandao wenu wa Tigo unawapenda na kuwajali sana, mnachotakiwa kufanya ni kufanya miamala na kujiunga na vifurushi kila wakati ambapo utabahatika kujishindia zawadi mbalimbali hata ile zawadi kubwa ya magari mawili, ambapo moja utampa umpendaye” amesema Mutalemwa.
Naye Diwani wa kata ya Bariadi Kija Bulenya akaishukuru kampuni ya Tigo kwa kumpatia zawadi kijana wa Bariadi ambapo kwake imekuwa mara ya kwanza kushuhudia mshindi akipewa zawadi.
“Ni furaha ilioje kwangu kuona mkazi wa hapa Bariadi akipewa pesa alizoshinda, huwa nasikia tu matangazo ya Magifti Dabodabo kwenye Runinga na Radio, nichukue fursa hii kwahamasisha wakazi wa Bariadi na nchi nzima kuendendelea kutumia huduma za Tigo kwa wingi” amesema Bulenya.
Kwa upande wake mshindi wa Magifti Dabodabo Robin Brasio ameishukuru Tigo kwa kumpatia kiasi hicho cha pesa na kusema atazitumia vizuri ili zilete tija maishani.
“Nitanunua bodaboda moja na kuifanya ya biashara ili iniingizie kipato, pesa zitakazobaki nitaongeza spea za pikipiki hapa katika duka langu ili niuze na kupata faida. amesema Brasio.
More Stories
Watoto wenye uhitaji wapatiwa vifaa vya shule
Wananchi Kisondela waishukuru serikali ujenzi shule ya ufundi ya Amali
RC.Makongoro ataka miradi itekelezwe kwa viwango