Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Mkuu wa kikosi cha poilisi cha usalama barabarani SACP Wilbroad Mutafungwa ameeleza kulizishwa  na hatua mbalimbali zinazochukuliwa na madereva wa mabasi na wenye maroli juu ya utii sheria bila shuruti juu ya kuhakikisha ajali za barabarani hazitokei .
Akiongea na waandishi wa habari mjini Kahama juzi akiwa kwenye oparesheni ya kuthibiti makosa hatarishi ya usalama barabarani aliyoanza toka Gairo hadi mikoa ya kada ya kati hadi ya kanda ya ziwa alisema amelizishwa na hatua mbalimbali zinazochukuliwa na wenye magari na madereva juu ya kuhakikisha ajari hazitokei.
Mutafungwa alisema oparesheni hiyo ya kukamata magari yanayovunja sheria na yanayobainika kuwa mabovu aliianza mei 11 katika barabara kuu ya rami kutoka Gairo kwenda mikoa ya kanda ya kati na ya ziwa ambapo ameeleza kulizishwa na hatua za madereva za utii wa sheria za usalama barabarani.
Alisema kwenye oparesheni hiyo toka tarehe hiyo amefanya ukaguzi wa mabasi ya abiria zaidi ya 173 kati ya hayo 87 yalifaata sheria na 47 yalikamatwa na kupigwa faini kwa sababu mbalimbali za kutotii sheria za usalama barabarani na madereva 9 walipewa onyo kali na mabasi 8 yalibainika na kosa la mwendo kasi.
Mutafungwa alisema katika ukaguzi huo mabasi 15 yalibainika kuwa na ubovu mbalimbali na kuyachukulia hatua za kisheria ikiwemo kuyasitishia safari hadi yafanyiwe matengenezo na pia alieleza kumekuwepo na mchezo mchafu unaofanywa na mabasi ya kuharibu sistimu ya kuonekana kwenye mfumo kudhibiti mwendo.
Kwa upande wa maroli ya mzingo alisema ametoa semina ya siku moja kwa madereva 67 katika kituo cha Misigiri kuhusu utii wa sheria za usalama barabarani ambapo amewataka wale wote wanaoendesha vyombo vya moto kutii alama za barabarani na wasitumie vileo na kuchana mwendo kasi na kuyapita magari mengine bila kuwa makini.
Mutafungwa alisema lengo la oparesheni hiyo ni kuhakikisha ajari za barabarani zinapungua ambapo ametoa wito kwa madereva na wenye magari , waendesha bodaboda kufaata sheria wanapoendesha vyombo vya moto kwa sababu anatamani siku moja pasiwe na askari barabarani bali sheria peke yake zifanye kazi.
More Stories
Mzumbe yaanika siri ya shahada udaktari wa heshima kwa Samia
Kujenga ofisi ya kisasa,akipewa ridhaa ya Uenyekiti
Ushiriki wa Rais Samia G20 wainufaisha Tanzania