December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Muswada marekebisho sheria nane wawasilishwa Bungeni

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma


MWANASHERIA Mkuu wa Serikali  Hamza Johari amewasilisha Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Na. 2 wa Mwaka 2024 ambao umelenga umelenga kufanya marekebisho katika sheria kuu nane.
Akiwasilisha Muswada huo Bungeni jijini Dodoma Johari amezitaja sheria hizo kuwa ni pamoja na Sheria ya Kuzuia Usafirishaji Haramu wa Binadamu Sura ya 432 Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai Sura ya 20  Sheria ya Serikali Mtandao Sura ya 273 na  Sheria ya Uhamiaji Sura ya 54.
Amezitaja sheria nyingine Sheria ya Ardhi Sura ya 113 , Sheria ya Bohari ya Dawa 70 ,Sheria ya Viwango Sura 30 na Sheria ya Tume ya Mipango Sura ya 127 /
Johari amesema  Sheria ya Kuzuia Usafirishaji Haramu wa Binadamu Sura ya 432, ambayo ilitungwa Mwaka 2008 na mpaka sasa imeshafanyiwa marekebisho mara tano.
Aidha  amevitaja vifungu vilivyopendekezwa kufanyiwa marekebisho katika sheria hiyo kuwa ni kifungu cha 3,17,30 31 32, vilevile Sheria hiyo inapendekeza kuongezwa kwa vifungu vipya vya 24A, 24B, 24C, na 24D.
“Mhe. Naibu Spika marekebisho yaliyopendekezwa yanalenga kutatua changamoto  zilizojitokeza wakati wa utekelezaji wa vifungu mbalimbali wa sheria hii na kuboresha vifungu hivyo ili kuimairisha Nyanza zote za kuzuia usafirishaji haramu wa binadamu”.amesema
Mwanasheria Mkuu wa Serikali amesema , Sheria ya Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai Sura ya 20, Sheria hiyo ilitungwa mwaka 1985 mpaka sasa imeshafanyiwa marekebisho mara 35, kifungu kinachopendekezwa kurekebishwa ni kifungu cha 205A kwa kuanisha namna muundo wa kuandaa ripoti ya uchunguzi wa Kifolensiki.
Aidha Mwanasheria Mkuu wa Serikali amesema Muswada huo unapendekeza kufanyika kwa Marekebisho katika Sheria ya Serikali Mtandao Sura ya 273 iliyotungwa Mwaka 2019 na haijawahi kufanyiwa marekebisho.
Amesema ,Sheria hiyo imefanyiwa Marekebisho katika kifungu cha 57 kinapendekezwa kurekebishwa ili kuongeza adhabu kwa kosa la kuondoa, kuharibu au kubadili data kumbukumbu za kielektroniki, mfumo au vifaa vya kielektroniki kwa lengo la Marekebisho haya ni kuhakikisha adhabu zinazowekwa zinazingatia uzito wa makosa.
Katika hatua nyingine Mhe. Johari ameitaja Sheria ya Uhamiaji Sura ya 54 ya Mwaka 1995 ambayo imefanyia marekebisho mara 12, Sheria hiyo imerekebishwa kwenye vifungu vya 3,20 23, 28, 32, 37, 46, 48 pia kuongezwa kwa kifungu kipya cha 8B na kifungu cha 42A, kifungu cha 11 kimepedekezwa kufutwa ili kuepusha mgongano wa kati ya Sheria ya Uhamiaji na Sheria ya
Tume ya Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Idara ya Uhamiaji Tanzania.
Johari amesema,Muswada wa huo unapendekeza kufanya Marekebisho katika Sheria ya Ardhi Sura ya 113, Sheria hii ilitungwa Mwaka 1999 na imefanyikwa marekebisho mara 14, kifungu cha 19 kinapendekezwa kufanyiwa marekebisho kwa lengo la kuweka utaratibu wa matumizi ya Ardhi kwa mtu aliepewa hadhi maalumu chini ya Sheria ya Uhamiaji, hata hivyo Serikali imependekeza marekebisho hayo kuondolewa ili yaendelee kufanyiwa kazi kwa kina zaidi.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali amezungumzia Marekebisho katika Sheria ya Bohari ya Dawa Sura ya 70 ya Mwaka 1993 ambayo imesharekebishwa mara 2, Muswada unapendekeza Marekebisho katika kifungu cha 16A, kwa lengo la kuongeza wigo wa uwekezaji wa Taasisi hiyona kuiwezesha kujiendesha kibiashara kwa kuzingatia maelekezo yatakayokuwa yanatolewa na Msajili wa Hazina na Mamlaka nyingine zinazohusika.
Vilevile amesema,Muswada huo unaopendekeza kufanyiwa Marekebisho katika Sheria ya Viwango Sura ya 130 iliyotungwa Mwaka 2009 na kufanyiwa marekebisho mara 1, Marekebisho hayo yanalenga katika vifungu vya 2, 4, 21A, 22, 23, 24, 27, 36. Marekebisho ya Sheria hii yanalenga kuimarisha utendaji kazi wa Shrika la Viwango nchini.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameendelea kwa kueleza kuwa Sheria ya Tume ya Mipango Sura ya 127 iliyotungwa Mwaka 2023, na inafanyiwa Marekebisho kwa mara ya kwanza, Sheria
hii inapendekezwa kwa ujumla katika masharti mbalimbali kwa kubadili jina la Tume na kuwa Tume ya Taifa ya Mipango kwa lengo la kuwianisha jina la Tume na wigo wa majukumu yake, pia kifungu cha 5 kimependekezwa kurekebishwa kwa kuongeza idadi ya wajumbe wanaoteuliwa na Rais kutoka wajumbe watano mpaka wajumbe nane.