June 18, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

MULIKA Tanzania yawanoa vijana matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii

Na Mwandishi wetu, Timesmajira

SHIRIKA linalohudumia vijana ambalo linajitahidi kuwaweka vijana katika kitovu cha michakato ya maendeleo na maamuzi MULIKA Tanzania limetoa mafunzo kwa vijana juu ya matumizi sahihi na salama kwa mitandao ya kijamii.

Akifungua mdahalo ulioenda sambamba na kutoa mafunzo ya usalama mtandaoni Jijini Dar es salaam mapema leo Juni 14,2023 Ofisa Mradi Mkuu wa Shirika hilo ,Marx Chocha amesema mafunzo hayo yataenda sambamba na maadhimisho ya siku ya mtoto wa afrika .

Chocha amesema katika mafunzo hayo vijana wamejadiliana na kupewa taarifa kutoka kwa wataalamu mbalimbali.”Tumeamua kutoa mafunzo haya kwa vijana kutokana kuwepo kwa changamoto kubwa zinazowakabili vijana katika mitandao ya kijamii,”amesema.

Amesema kwa mujibu wa takwimu zinaonesha kuwa watanzania wengi wanatumia huduma za mtandao huku vijana wakiongoza ambapo vijana wengi wamekuwa wahanga wa kusababisha changamoto mbalimbali na kueleza kuwa taarifa zao nyingi wakipata katika mitandao ya kijamii.

“Kupitia mafunzo haya tutawapa elimu ya ujuzi na uelewa juu ya kufanya maamuzi salama sambamba na kupitia Sheria mbalimbali na hatimaye kuwa sehemu salama wanapokuwa katika mitandao”amesema.

Aidha amesema wakifanya tafiti kupitia mitandao ambapo waliweza kubaini kuwa na wigo wa kiasi gani cha matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii.

Akiwasilisha mada katika mafunzo hayo Mhariri Mkuu wa Kituo cha Television na Redio Clouds , Joyce Shebe amesema uhuru wa kujielezea unatoa fursa kwa watu kuwasilisha na kuonesha uwajibikaji.

Aidha amewaomba vijana hao kutumia uhuru wa kujieleza ili kujenga jamii yenye uwajibikaji.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya ya Nukta Afrika, Nuzulack Dausen amesema kuwa na taarifa sahihi ni muhimu katika kudai haki na uwasilishaji.

Nae mmoja wa vijana hao Mary Mbago amesema elimu ya masuala ya matumizi sahihi na salama kwa mitandao ya kijamii ni muhimu kwanj vijana wengi wamekuwa wakiitumia katika masuala mbalimbali ikiwemo biashara na kupata fursa mbalimbali.