Na Israel Mwaisaka,TimesMajira Oline,Nkasi
MTOTO Aizeck Chipuntwa (2) mkazi wa kijiji cha Lunyala wilayani Nkasi mkoani Rukwa amefariki baada ya kutumbukia kwenye kisima.
Tukio hilo limetokea jana majira ya saa 8, mchana, kijijini hapo ambapo mama wa mtoto huyo Priska Mbilingi amesema kuwa kabla ya tukio hilo,alikwenda dukani kununua zawadi kwa ajili ya kuepeka kwenye harusi ambapo alimuacha mtoto huyo akiwa nje aakicheza.
Akizungumza kwa uchunhu na Majira mama huyo amesema kuwa baada ya kurujea alishangaa kutomuona mtoto huyo ndipo alipoanza kumtafuta kila kona ya nyumba hiyo bila mafanikio.
Amesema kuwa walishirikiana na ndugu pamoja na majirani kumtafuta kwa muda mrefu lakini hawakuweza kumuona.
Afisa mtendaji wa kijiji hicho cha Lunyala Esel Mgonzo amesema kuwa kupata taarifa za kutafutwa kwa mtoto huyo alishirikiana na majirani kuanza kumtafuta kila kona katika kijiji hicho.
Amesema kuwa wanakijiji walionyesha ushirikiano mkubwa katika kumtafuta mtoto huyo ambapo jana saa 9 mchana walimkuta kwenye kisima cha maji kilicho karibu na nyumba hiyo akiwa amekufa.
Afisa mtendaji huyo amesema kuwa walitoa taarifa Polisi ambao walifika eneo la tukio na baada ya uchunguzi ndugu waliruhusiwa kuuchukua mwili wa marehemu na kuendelea na taratibu za mazishi.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Mkuu wa Wilaya Nkasi Said amesema kuwa Serikali imekuwa ikitoa elimu kuhusiana na kuvijengea na kuvifunika visima vyote vilivyo kwenye makazi ya watu ili kuepuka madhara.
Mkuu huyo wa wilaya amemuagiza Afisa Tarafa ya Namanyere kwenda katika kijiji hicho na kuzungumza na wananchi juu utekelezaji wa maagizo ya Serikali juu ya kufunika visima vyote vilivyo kwenye makazi ya watu ikiwa ni pamoja na kufukia mashimo yote na madimbwi ambayo ni hatarishi kwa watoto hasa katika kipindi hiki cha mvua
More Stories
CCM hakuna kulala, Nchimbi atua Tabora kwa ziara ya siku mbili
Kongamano la Uwekezaji na Biashara lafunguliwa Pwani
Rais Samia afurahia usimamizi mzuri wa miradi