December 29, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mtemvu: Waliokosa uwezo waondolewe

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Abas Mtemvu, amesema chama Mapinduzi CCM ndani ya chama hicho amna maboya kama yapo ameomba yaondolewe .

Mwenyekiti Mtemvu aliyasema hayo kata ya GONGOLAMBOTO Wilayani Ilala wakati Diwani Lucas Lutaunurwa akiwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya mwaka 2020/2022.

“Katika chama changu amna maboya wote waliochaguliwa Wana uwezo wa kukipeperusha chama cha Mapinduzi CCM 2024 katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa pamoja na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 kama yapo maboya yalipita kwa kushinikizwa kwa ajili ya mtu naomba yaondolewe ” alisema Mtemvu .

Mtemvu alisema CCM inataka watu waliomba wenyewe Ili wakisaidie chama na Serikali katika uongozi wao .Alisema dhumuni la ZIARA hiyo ya kupokea kila Mwaliko ni kuangalia VIONGOZI waliochaguliwa kama Wana uwezo wa kuongea na kukisaidia chama.

Alitumia nafasi hiyo kupongeza utekelezaji wa Ilani ya ccm ya kata ya GONGOLAMBOTO iliyowasilishwa na Diwani Lucas Lutainurwa ambapo katika kata hiyo Kuna uwekezaji mkubwa wa Miradi ya MAENDELEO ambayo inatekelezwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Rais Samia Suluhu Hassan .

Alisema kila Diwani akiwasilisha taarifa awape Mwaliko Wajumbe wa Mashina ,Wenyeviti wa Serikali za Mitaa na wana CCM Ili waone Serikali unavyofanya kazi .

Akizungumzia Mikopo ya Serikali alisema Watu wanaoitaji Mikopo ya Serikali ya wapewe watakaonyimwa Mikopo apewe taarifa Ili aweze kuchukua hatua kwani sifa ya KIONGOZI kutumikia wananchi Dar es Salaam ni sehemu ya kazi kama Kuna mtu awezi kufanya kazi katika Mkoa huo apewe Taarifa .

Aliwataka Wana CCM wapendane na kutekekeza Ilani wakiwasilisha taarifa za Utekelezaji wa Ilani ya chama wawape Mwaliko viongozi wa Serikali waje kujibu kero zao .

Wakati huo huo aliwataka watangaza Nia katika uongozi 2024 na 2025 wasubiri Muda bado mpaka filimbi ianze kulia badala yake wote wapendane na kujenga chama .

Mwenyekiti wa CCM Mkoa Dar es Salaam Abas Mtemvu akisalimiana na Diwani wa Gongolamboto Lucas Lutaunurwa Leo wakati Diwani Lucas akiwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya ccm Picha na HerI Shaaban.
Mbunge wa Jimbo la Ukonga Jerry Silaa akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa Dar es Salaam Abas Mtemvu Kata ya Gongolamboto wakati Diwani Lucas alipokuwa akiwasilisha taarifa ya utekekezaji wa Ilani (katikati )Katibu wa CCM wilaya ya Ilala Idd Mkowa (Picha na Heri Shaban ).
Mwenyekiti wa CCM Mkoa Dar es Salaam Abas Mtemvu akikagua miradi ya Maendeleo shule ya Msingi MIKONGENI English Medium iliyopo Gongolamboto Wilayani Ilala ,wengine Mbunge wa Jimbo la Ukonga Jerry Silaa ,Katibu wa CCM Wilaya hiyo Idd Mkoa na Diwani wa Gongolamboto Lucas Lutainurwa (Picha na Heri Shaaban )