Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala
Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam Abas Mtemvu, amewataka Wenyeviti wa Serikali za Mitaa kuwa Wasafi katika utekelezaji wa Majukumu yao Pamoja na kuwa na mahusiano mazuri Jamii .
Mwenyekiti Abas Mtemvu ,aliyasema hayo Kata ya Zingiziwa wakati Diwani wa Maganga Maige akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM .
“Wenyeviti wa Serikali za Mitaa naomba muwe waminifu mjiepusshe na migogoro ya uvamizi ya ardhi katika mitaa yenu mnaelekea katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 mazuli uliochuma kwa Wananchi ndio utakayovuna muwe Wasafi Ili muweze kujiuza pamoja na kukiuza chama ” alisema Mtemvu .
Alisema Mwenyekiti yoyote anayetaka kuendelea lazima awe msafi asiwe na makando kando nikimaliza ziara ya kuzunguka Mkoa Dar es Salaam ataanza ziara kwa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa na kuuliza Mikutano ya Wananchi kama inafanyika ikiwemo mapato na Matumizi .
“Naomba mwaka 2024 tusimamishe Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa anayejiuza kutokana na kazi zake naomba Wenyeviti mjishushe mtekeleze Ilani kwa vitendo katika kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwemo kusemea mazuri ya Rais ikiwemo Utekelezaji wa Ilani ya Chama ” alisema .
Wakati huo huo alisema ataleta Wataalam kwa ajili ya kurathimisha maeneo ya ardhi Ili Kila Mwananchi aweze kupata Hati yake aweze kukopesheka na kuchukua mikopo.
Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la DAR es Salaam Ojambi Masaburi alimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anajenga chama Cha Mapinduzi na kuwatumikia vyema watanzania .
Naibu Meya alisema Miradi ya maendeleo Ilala inakuwa kwa kasi sana kwa usimamizi wa Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la DAR es Salaam na mambo yote yanayofanyika Kata ya Zingiziwa ni ushirikiano wa madiwani wa Jiji kupeleka maendeleo katika katika Zingiziwa .
Wakati huo huo Naibu Meya Masaburi alimpongeza Diwani Maige kwa kukomboa Mtaa wa Ngobedi katika mgohoro wa Mpaka wa Kisarawe na Ilala mpaka Diwani Maige aliwekwa ndani kwa ajili ya kutetea ardhi ya Wananchi wake wawe Ilala wasisomeke Kisarawe na hatimaye alifanikiwa baada maelekezo ya Serikali Zingiziwa wakashinda.
Mwenyekiti wa CCM WIlaya ya Ilala Said Sidde aliwaoongeza Zingiziwa kwa kumpa ushindi mkubwa wa chama Cha Mapinduzi mpaka amechaguliwa kuwa Mwenyekiti .
.Mwenyekiti Sidde alisema kata ya Zingiziwa ni ya Wazawa Wazalamo ndio wengi wapo Kata hiyo ikiwemo Nyasa mpaka kwa Makamu wa Rais .
Mjumbe wa Mkutano Mkuu CCM Taifa MNEC Simba Juma Gadafi alipongeza Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuwekeza miradi ya Maendeleo Kata ya Zingiziwa ikiwemo Sekta ya Afya na Barabara na Sekta ya Elimu .
MNEC Juma Simba Gadaf alitumia nafasi hiyo pia kumpongeza Naibu Meya Masaburi kwa Sasa ameiva kisiasa ana Mahusiano mazuri na Madiwani wenzake wa Halmashauri kwa ushirikiano .
More Stories
Kiswaga:Magu imepokea bilioni 143, utekelezaji miradi
Zaidi ya milioni 600 kupeleka umeme Kisiwa cha Ijinga
Kamishna Hifadhi ya Ngorongoro atakiwa kupanua wigo wa Utalii nchini