December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mtanzania aomba Watanzania wampigie kura ashinde taji la Miss/ Mrs Africa

Na Mwandishi Wetu, TimesmajiraOnline, Uingereza

MTAZANIA anayeishi Uingereza, Alice Gyunda ni miongoni mwa washiriki 20 kutoka nchi mbalimbali za Afrika waliofanikiwa kuingia kwenye kinyang’anyiro cha kuwania taji la  miss /mrs Africa

Ushindi wa shindano hilo unatokana na namna mshirika anavyopigiwa kura kupitia website ya https//afrikaukpageants. co. uk/poll/mrs-missafrica-finalist-2023.

Hata hivyo, bado nguvu ya Watanzania kumpigia kura Mtanzania huyu imekuwa ni ya ndugu tofauti na namna ya ushiriki wa taifa jirani la Uganda, ambapo wananchi wajitokeza kwa wingi kumpigia kura mshiriki wao.

Kutokana na changamoto hiyo mshiriki, Alice gyunda amewaomba Watanzania kutoka nchi mbalimbali kushiriki kumuunga mkono kwa kupimpigia kura nyingi za ndiyo kupitia link iliyoanishwa hapo juu.

Amesema ushindi wake ni fursa kwa Watanzania ambapo kwa mujibu wa zawadi zilizoanishwa kwenye shindano hi pamoja na mshindi atakayetwaa taji hilo atapata fursa ya kuandika andiko la namna atakavyosaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu katika nchi yake ya uraia.

Hadi sasa ni asilimia sita ya upigaji kura wa Watanzania katika shindano hilo, huku mshiriki wa Uganda akiongoza kwa asilimia 39 huku akiwaacha mbali washiriki wengine akiwamo, Alice Gyunda.



Hadi sasa tayari mtanzania huyo ametoa msaada wa vitu mbalimbali kwa watoto wanaoishi katika mazingira  magumu katika halmashauri ya Mkuranga, ikiwamo unga, sabuni, mchele, mafuta ya kula  ili kusaidia makundi hayo.



Alice ambaye taaluma yake ni mwalimu kabla ya kwenda kuishi ughaibuni akiwa amewahj kufundisha katika shule ya msingi Kawe na Oysterbay.

Pia mshiriki huyo ana kipaji cha usanii wa sanaa ya nyimbo zenye maudhui ya uelimishaji, lakini malengo yake kama Watanzania watampigia kura na kushinda ana mpango wa kuanzisha vituo vya kuibua vipaji kwa wasanii wa sanaa ya muziki kila mkoa

Amesema kupitia vituo hivyo vya kuibua vipaji kwa watoto pia vitakuwa na mkakati endelevu wa kutunza wasanii watakaopatikana katika vituo hivyo kwa kuwawezesha kupata taalum ya sanaa ya muziki

Amesema uanzishwaji wa vituo vya uibuaji vipaji vitakavyoanzishwa vitakamilika katika sekta zote za uwepo wa studio za kisasa kwa ajili ya kurekodi nyimbo, ambapo pia kwa wasanii watakaofanya vizuri wataunganishwa kufanya mziki wa pamoja na wasanii wakubwa wa Tanzania ikiwamo ulaya na Afrika.

Amesema lengo la kuanzisha vituo hivyo vya kuibua vipaji ni kutaka kuandaa wasanii wengi wakubwa wa muziki wa bongo flavor , hip poo, singeri na rage.