November 9, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mtandao wa TECMN wazindua ripoti ya Kutokomeza Ndoa za Utotoni

Na Mwandishi wetu, Timesmajira online

MTANDAO wa Kutokomeza Ndoa za Utotoni (TECMN) unaojumuisha mashirika 69 umeiomba Serikali kuzingatia kile kilichoelezwa na Mahakama ya Rufaa juu ya Sheria ya ndoa za utotoni ya mwaka 1971 ili kuweza kuharakisha mchakato wa maboresho ya Sheria.

Hayo yamebainishwa jiji Dar es salaam na Mjumbe wa bodi ya mtandao huo , Dkt Hellen Kijo Bisimba wakati wa uzinduzi wa ripoti ya ndoa za utotoni ambayo imeandaliwa na TECMN.

Amesema pamoja na Mahakama ya Rufani kuagiza kubadilishwa kwa sheria hiyo ambayo ni kandamizi kwa watoto bado Serikali imeendelea kukaa kimya.

“Sisi kama wanamtandao tunaamini katika nguvu za moja katika kusimamia masuala mbalimbali ni miaka mitatu sasa tangu hukumu hiyo itolewe …tunaiomba Serikali iweze kubadilisha ili tuwe na mfumo wa sheria inayolinda watoto”amesema Dkt Kijo Bisimba

Kwa upande wake Mratibu wa mtandao huo Euphonia Edward ambaye amezungumzia ripoti hiyo
amesema imeangazia safari yao tangu kuanza kwake miaka 10 sambamba na kuonesha wito wao kwa jamii.

“Tunaelekeza nguvu katika kupambana na ndoa za utotoni tatizo la ndoa za utotoni bado linachangamoto katika jamii”amesema Euphonia

Na kuongeza kuwa
“Lengo kuu ni kuwa na sauti moja pamoja na kuweka ajenda ya Kutokomeza ndoa za utotoni kama kipaumbele chetu”alisisitiza

Naye Wakili kutoka Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) Barnabas Kaniki amesema ni wakati muafaka wa wabunge kuhoji ni lini muswada wa mabadiliko ya sheria hiyo utapelekwa Bungeni.

Mratibu wa mtandao Kutokomeza ndoa za utotoni (TECMN) Euphonia Edward akizungumza na waandishi kuhusu ripoti ya Kutokomeza ndoa za utotoni
Katikati ni Mjumbe wa Bodi ya TECMC Dkt Hellen Kijo Bisimba akiwa pamoja na wajumbe wakiwameshika ripoti ya Kutokomeza ndoa za Utotoni baada ya kuzinduliwa