Na Mwandishi wetu, Timesmajira Online GEITA
KAMANDA wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita, Safia Jongo amepiga marufuku tabia ya baadhi ya Askari kuomba rushwa pale ambapo Mtuhumiwa anapokamatwa na kupewa dhamana na Ndugu zake kwa kumtaka atoe chochote katika Vituo vya Polisi.
Akiongea na Wakazi wa Kata ya Kamoge Wilayani Bukombe Mkoani Geita Katika ziara aliyofanya Mkuu wa Mkoa wa Geita Martin Shigella, Jongo amesema ni marufuku Mwananchi kutoa kitu chochote kwa Askari endapo Mtuhumiwa atapewa dhamana na Ndugu zake kwa kutimiza Masharti.
“kuingia Polisi bure kutoka hela hili jambo marufuku mbele ya Uongozi wangu Mimi Bibi yenu, ukiingia Polisi bure kutoka bure, wewe ukitoa hela umetoa rushwa na sitakubali nawaachia namba yangu ya simu mniambie huyo Askari anayedai hela kutoka ndani ya kituo cha Polisi Mimi sasa hivi nimehama kwenye Ubibi nitakuwa Shangazi”
RPC Jongo amesema baadhi ya Askari wamekuwa wakilichafua Jeshi la Polisi huku akiahidi endapo watagundulika atawachukulia hatua za Kisheria huku akiwataka Wananchi kutoa taarifa mapema kwa atakayeendelea kufanya hivyo.
More Stories
Kamati ya Mfuko wa Jimbo Musoma Vijijini yagawa vifaa vya ujenzi
Hatma mrithi wa Kinana kupatikana
Mrithi wa Kinana CCM kujulikana katika Mkutano Mkuu wa Jan 18/19