December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Msiruhusu Mgeni kulala na watoto

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

Jumuiya ya Wazazi Kata ya Ilala imetoa onyo kwa wazazi wasiruhusu watoto wao kulala na Mgeni chumba kimoja kwa ajili ya kuwaepusha wasifanyiwe vitendo vya ukatili usiku .

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Kata ya Ilala Sabry Abdalh Sharif ,alisema hayo katika ziara ya Jumuiya hiyo kuwashukuru wanachama Kila Matawi baada kumalizika Uchaguzi .

“Mimi na kamati yangu ya Utekelezaji ya Jumuiya Wazazi Kata ya Ilala tumepita Kila Tawi kuwashukuru wanachama wetu ndio dhumuni la ziara ,pia tunatoa onyo kwa Wazazi wasiwamini wageni ndugu zao kulala chumba kimoja na Watoto usiku ni mwingi anaweza kumfanyia vitendo vya ukatili vikiwemo vya ubakaji “alisema Sabry .

Mwenyekiti Sabry alisema Jumuiya ya Wazazi Ilala imefanya ziara katika shule mbalimbali zilizopo Ilala wamekutana na changamoto mbalimbali za Wanafunzi zikiwemo vitendo vya ukatili ambayo wanafanyiwa Wanafunzi.

Alisema suala la malezi kwa watoto shuleni ni changamoto katika kusimamia watoto wetu wazazi wamekuwa nyuma kuwachia Walimu peke yao amewataka wazazi washirikiane na Walimu katika malezi .

Mwenyekiti Sabry alisema katika ziara ya sekta ya Elimu wamebaini Watoto wapo juu wazazi chini na kesi za ubakaji zimekuwa nyingi .

Akizungumzia JUMUIYA ya Wazazi aliwapongeza kwa kumaliza chaguzi na kushinda kwa kishindo amewataka viongozi wa matawi kushirikiana na chama cha mapinduzi katika kujenga chama kiweze kufikia malengo yake .

Aliwapongeza JUMUIYA ya Wazazi tawi la Ilala kuongeza wanachama alisema watashirikiana nao Ili kuwasajili kuongeza mapato ndani ya JUMUIYA ya Wazazi .

Diwani Aisha Kipini wa Viti Maalum wanawake Ilala, aliwataka Wazazi wawe karibu na Walimu Shuleni suala la malezi ni jukumu letu badala yake wasiwachie wanafunzi Walimu peke yao .

Aliwataka Wazazi kuweka utaratibu wa kuwakagua Watoto wao wa kiume na wakike wasiwaope.

Katika hatua nyingine Diwani Aisha amewataka wababa wakifanyiwa Ukatili na mama Nyumbani wafunguke wasikae kimya madawati ya kijinsia yapo hivyo Wana jukumu la kwenda KUTOA Taarifa .