December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Msigwa:Maisha yana mambo mengi ni muhimu kujifunza vitu vingi

Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma

KATIBU Mkuu Wizara ya Utamaduni,Sanaa na Michezo, na aliyewahi kuwa Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa idara ya Habari Maelezo  Gerson Msigwa amesema ni muhimu kujifunza vitu vingi kwani maisha yana Mambo mengi.

Msingwa ameyasema hayo Mara baada ya kutunukiwa Shahada ya Umahili wa Usimamizi wa Biashashara na kuahirishwa kwa Mahafali ya 14 ya Chuo cha  St. John’s yaliyofanyika mapema leo,Desemba 1,2023 hii Jijini Dodoma.

Na kuongeza kuwa kama mtu atasalia na Jambo moja pekee anaweza kujikuta kama amejifungia katika chumba.

“Nadhani ni muhimu kujifunza vitu vingi kwasababu maisha yana Mambo mengi ukibaki kwenye Jambo moja pekee umejifungia kwenye chumba kumbe kuna fursa zingine nje ya kile ulichosomea kama mimi nulivyotoka kwenye Tasnia ya Uandishi wa Habari na kwenda katika Tasnia ya Usimamizi wa Biashashara,

“Ni vizuri kubobea kwenye kitu kimoja ila ni vizuri zaidi angalau kuvijua vitu kadhaa ili unapokutana na changamoto tofauti uwe unaweza kuzimudu na hiki ndicho ambacho Mimi nimekifanya,”amesema.

Pia ameeleza sababu zilizomfanya kusoma  kozi hiyo ya Umahili wa Usimamizi wa Biashashara amesema anaamini itampa Umahili katika utendeji wake wa Kazi ili kuondokana mazoea kama wengi wanavyofanya.

“Mimi nilifanya hivi kwasababu nilihitaji Sana kusomea kozi ambayo itanipa Umahili katika utendeji wangu wa Kazi hasa kufikiria kibiashara katika shughuli zetu kwangu Mimi naona hii ni moja ya changamoto ambazo katika Utumishi Umma tunazo na wengi tunafanya Kazi kwa mazoea”.

“Kozi imenifundisha kufanya Kazi kwa malengo,kuheshimu muda na kufanyakazi kwa matokeo n hili ndo Jambo kubwa nililotamani nilipate pamoja na kwamba lilikuwa nje kidogo na Uandishi wa Habari ambayo ndiyo hasa nyumbani kwangu,iliniongezea thamani kubwa kwenye Uandishi wangu na kuongeza thamani kubwa katika Utumishi wangu”.

Pia Katibu Mkuu huyo amesema kuwa katika kozi hiyo ya Umahili wa Usimamizi wa Biashashara amejifunza kufanyakazi kimkakati,kufanya Tafiti ambalo ni Jambo muhimu katika uandishi wa Habari na Mawasiliano kwani ni lazima mtu kufanya utafiti.

“Nimepata Umahili katika Usimamizi wa Biashashara,ambapo katika Usimamizi wa Biashashara nimejifunza kufanya Kazi kimkakati,kufanya Tafiti Jambo ambalo ni muhimu katika Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwani ni lazima watu tuwe tunafanya Tafiti,

“Kumekuwa na changamoto katika Tasnia ya Uandishi wa Habari kufanya Jambo bila Tafiti matokeo yake unafanya vitu kwa kubahatisha hivyo kozi hii imenifundisha hayo pia”.

Hii ni Mahafari ya 14 tangu kuanzishwa kwa Chuo cha St John Tawi la Dodoma na jumla ya wahitimu 998 wamehitimu katika kozi mbalimbali huku kikiwa kimeshatoa wahitimu zaidi ya 17,000 toka kuanza kwake.