Na Mwandishi wetu, Timesmajira Online
SHIRIKA linalotetea Haki za Wasichana Tanzania (Msichana Initiative) limelaani vikali tukio la kujinyonga kwa Rebecca Benjamin(17) mkazi wa kata Izunya Wilaya Nyang’hwale Mkoani Geita kutokana na msongo wa mawazo uliosababishwa na athari za kuolewa katika umri mdogo.
Akisoma tamko la kulaani tukio hilo mbele ya waandishi wa habari jiji Dar es salaam leo Februari 18 Mkurungezi Mtendaji wa Shirika hilo Rebeca Gyumi amesema tukio hilo linaonesha ni kwa kiasi gani ukatili kwa watoto bado ni mkubwa katika jamii.
Amesema ukosefu wa elimu juu ya madhara ya ndoa za utotoni katika jamii kuanzia ngazi ya jamii hadi ngazi ya juu bado ni mkubwa ikiwemo sura ya ukatili kwa watoto kutozungumziwa vya kutosha.
“Rebecca amefariki dunia baada ya kujinyonga hadi kupoteza maisha kwa kutumia kamba iliyosukwa kwa chandarua kwenye kenchi ya nyumba yake, chanzo alikuwa akilalamika kwamba kwanini kila akiolewa anaachika na tayari alikuwa ameishaachika mara tatu kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoani Geita , Henry Mwaibabe “amesema Gyumi
Na kuongeza kuwa “Rebecca ni mtoto kama tusingehamasisha tamaduni ambazo hazioni suluhisho la umasikini wetu ni kuoza wasichana au kuona thamani yao inaendana na kuwa kwenye ndoa yamkini mtoto Rebecca asingefikia hapa”alisisitiza Gyumi
Gyumi ameendelea kueleza kuwa tukio hilo ni latatu kutokea baada ya lile lililotokea katika mkoa wa songwe, Kijiji cha Ilanga kata ya mlale likimuhusisha mtoto wa miaka 16 kisha kumchoma na kumtupa kwenye korongo na jingine Kigoma.
“Pamoja na matukio haya kuendana na wimbi la matukio ya watu kuuwa ama kujinyonga bado yamekuwa yakionesha sura ya ukatili kwa watoto kutozungumzwa vya kutosha”amesema
Aidha alitoa wito kwa wabunge na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuchukua jukumu hilo sasa la kubadilisha Sheria ya ndoa ya mwaka 1971 kifungu cha 13 na 17 ambavyo vimekuwa vikiruhusu wasichana kuolewa wakiwa na umri wa miaka 14 kwa ridhaa ya mahakama .
Gyumi amesema licha ya Serikali kurudisha mchakato huo wa mabadiliko Sheria kwa wananchi kutaweza kusababisha kuchelewa mchakato .
“Kwa dhamana waliyopewa wabunge wetu kikatiba, mchakato huu unafanya Bunge kukwepa jukumu lake la muhimu la kuwalinda watoto na ndoa za utotoni”amesema Gyumi.
Mkurungezi huyo aliipogeza jitihada zinazofanywa na Serikali kupitia tamko na waraka na mwongozo wa wanafunzi waliokatisha masomo kurudi shule na kueleza kuwa ina wasiwasi kuwa inawezekana kukaziba dirisha na kuacha mlango wazi kwa kuendelea kuacha Sheria inayoruhusu watoto kuolewa.
Hata hivyo alivitaka vyombo vya Sheria kuchukua hatua za kisheria kwa wahusika wote ikiwemo wazazi na waliohusika kumuozesha binti huyo kuanzia ndoa ya kwanza mpaka ya tatu
More Stories
CPA.Makalla :CCM kutumia 4R za Rais Samia katika uchaguzi Serikali za Mitaa
CCM kutumia 4R za Samia Uchaguzi Serikali za Mitaa
Dkt. Mpango awasilisha salam za Rais Samia mazisha Baba yake mzazi, Gavana Tutuba