Na mwandishi wetu, TimesMajira Online
Washindi wengine akiwemo wa Mil.20 na Mil.10 wakabidhiwa fedha zao
• Jumla ya shilingi milioni 114 zimetolewa pamoja na gari 1 aina ya Toyota Rush kwenye Kampeni ya Ndinga la Kishua
Kampeni ya Ndinga la Kishua iliyoendeshwa na kuratibiwa na kampuni ya mawasiliano Tigo, imekabidhi gari aina ya Toyota Rush kwa mshindi wa Ndinga la Kishua kutoka Kahama na washindi wengine wawili kutoka Dar es Salaam, walioibuka na Mil 20 na Mil 10 wiki iliyopita na kufanya idadi ya washindi wa fedha taslim waliopatikana kupitia promosheni hii iliyodumu kwa wiki nane (8) kufikia sabini (70).
Kampeni hii ya “Ndinga la Kishua” ilianza rasmi mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka jana na kumalizika tarehe 18 Januari 2023.
Pamoja na kupokelewa vizuri na wateja wa Tigo Pesa na kufanikiwa kubadilisha maisha ya watanzania wengi kwa kuwafanya mamilionea, kampeni hii pia imechangia kuongezeka kwa miamala ya Tigo Pesa, kuongeza wateja wa Tigo Pesa na kuimarisha baadhi ya huduma ikiwemo ulipiaji wa bidhaa na huduma kupitia Lipa kwa Simu na malipo ya Serikali.
Ikumbukwe kuwa promosheni hii ilikuwa ni mchongo wa tatu wa Kampeni ya Wakishua ambayo ilizinduliwa jijini Dar es Salaam Septemba 2022 ambapo wateja wa Tigo Pesa walinufaika na zawadi mbalimbali ikiwemo safari iliyolipiwa kila kitu, ya kwenda Qatar kutazama mechi za kombe la dunia mubashara, muda wa maongezi pamoja na vifaa vya nyumbani vya Hisense.
Tunapohitimisha kampeni hii ni dhahiri kuwa washindi wa leo wamebahatika kujishindia zawadi kubwa kabisa kupitia droo iliyofanyika wiki iliyopita, zawadi hizo ikiwa ni pamoja na fedha taslim Milioni 20, Milioni 10 na gari mpya aina ya Toyota Rush ambapo mshindi wa gari ni Samson Daniel Samson, kutoka Kahama,na mshindi wa Mil.20 ni Kanana Abdallah Hamudi kutoka Chanika,Dar es Salaam na Mshindi wa Mil.10 ni James Gabriel Mwala.
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi zawadi hizo kwa washindi hao Afisa Mkuu wa Tigo Pesa, Angelica Pesha alisema
“leo tunawatambulisha kwenu na kuwakabidhi zawadi washindi wetu walioibuka kidedea kwenye kampeni yetu ya “Ndinga la Kishua “ iliyodumu kwa wiki nane. Lengo letu kama kampuni ni kutoa huduma za kibunifu za kifedha kwa kila mtanzania nchi nzima. Na kupitia kampeni hii tumeona mwamko mkubwa sana wa watanzania kufanya miamala yao ya kila siku kidigitali kupitia Tigo Pesa. Pia, tumeona jinsi kampeni hii ilivyosaidia watanzania waliojipatia mamilioni wanavyotimiza ndoto zao, tunafarijika kuona kampuni yetu inawezesha yote haya”.
Aliongeza kuwa washindi hao wamepatikana ikiwa ni baada ya kufanya miamala kwa wingi kwa njia ya Tigo Pesa ambapo ili wateja waweze kushinda pesa taslimu au Toyota Rusha mpya walitakiwa kufanya miamala mbalimbali kwa Tigo Pesa na kuifanya Tigo Pesa kuwa ya kwanza kila wanapotaka kufanya miamala. Kwa upande wa mshindi wa Toyota Rush Samson anasema, huku akiwa na tabasamu.
Ikumbukwe kuwa kampeni ya “Ndinga la Kishua” ilianza toka mwaka jana mwezi Novemba ambapo wateja wa Tigo Pesa 70 waliibuka washindi wa pesa taslimu zaidi ya milioni 114 na mshindi 1 aliibuka mshindi wa gari jipya aina ya Toyota Rush lenye thamani ya shilingi milioni 78.
More Stories
Kiswaga:Magu imepokea bilioni 143, utekelezaji miradi
Zaidi ya milioni 600 kupeleka umeme Kisiwa cha Ijinga
Kamishna Hifadhi ya Ngorongoro atakiwa kupanua wigo wa Utalii nchini