Na Heri Shabaan, TimesMajira Online
MWENYEKITI wa Serikali ya Mtaa Mafuriko Ilala Ally Mshauri ,amewataks wanafunzi wa darasa la saba shule ya Msingi Ilala kufaulu wote katika mitihani yao ya Taifa ya Elimu msingi.
Mwenyekiti AlLLY MSHAURI alifanya ziara na Wajumbe wake wa Serikali ya Mtaa Mafuriko kata ya Ilala kutembelea shule ya Msingi Ilala kuonana na wanafunzi wa darasa la saba wa shule hiyo ambao wanatarajia kufanya mitihani yao ya Taifa ya kuhitimu elimu ya msingi mwaka 2024 na kuwapa moyo wakiwataka wafaulu wote.
Akizungumza na wanafunzi wa shule hiyo Mwenyekiti Ally Mshauri aliwapa moyo wanafunzi wa shule hiyo na kuwataka wajiandae vizuri katika mitihani yao ya Taifa wasiwe na wasiwasi wakiwa Darasani kwani masomo waliosoma ndio mitihani iliyotungwa na Serikali.
“Serikali ya Mtaa Mafuriko inawapenda sana wanafunzi wetu sisi Serikali ya Mtaa Mafuriko ni walezi wa shule hii tumekuwa tukishirikiana na uongozi wenu wa shule kwa ajili ya chakula cha wanafunzi siku za mitihani kwa kutoa chakula bure bila Wazazi wenu kuchangia miaka yote ofisi yetu ya Serikali ya Mtaa inawaombea wote mfaulu “alisema Mshauri.
Mwenyekiti Mshauri aliwataka wanafunzi watenge muda wa kujisomea nyumbani mara baada vipindi vya masomo kumalizika waache kuzurula na kutega kwenda shule.
Aidha Mshauri alisema wanaunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan, katika sekta ya Elimu katika kuwaandalia mazingira bora wanafunzi wa shule za Msingi na shule za awali waweze kupata elimu bora.
Mitihani ya kuhitimu elimu ya msingi mwaka 2024 inatarajia kufanyika mwezi September .
More Stories
Watakaokwamisha mapato Kaliua kukiona cha moto
Dkt.Gwajima aagiza kuundwa kamati za ulinzi wa watoto
Kilo 673.2,dawa za kulevya zakamatwa Bahari ya Hindi