Na Jackline Martin, TimesMajira Online
BOHARI ya Dawa (MSD) imeimarisha mfumo wa usambazaji bidhaa za afya mara sita kwa mwaka (Kila baada ya miezi miwili) kwa mwaka wa fedha 2022/23 badala ya mara nne kwa mwaka (miezi mitatu) hivyo kupunguza muda wa vituo vya afya kusubiri bidhaa za afya
Akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari jana Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu MSD, Mavere Tukai, alisema wamefanikiwa kununua matrela 16 yenye thamani ya sh. Bilioni 2.6 ili kuongeza kasi ya usamabaji wa bidhaa hizo.
Alisema wamefanikiwa kuongeza usamabazaji wa bidhaa za afya kwa asilimia 16 kutoka sh. Bilioni 320 kwa mwaka wa fedha 2021/22 hadi sh. Bilioni 373 kwa mwaka wa fedha 2022/23.
Kuhusu ununuzi wa bidhaa za afya. Tukai alisema wamefanikiwa kuanzisha kitengo maalumu cha usimamizi na ufuatiliaji wa mikataba
“Ununuzi wa bidhaa za afya kutoka kwa wazalishaji wa ndani umeongezeka kutoka sh. Bilioni 14. 1 mwaka wa fedha 2021/22 hadi kufikia sh. Bilioni 39.77,” alisema.
Pia Tukai alisema kwa sasa hawaagizi tena bidhaa kutoka nje ya nchi, zile ambazo zinakidhi vile ambazo zinakidhi mahitaji na viwango vya ubora hivyo kutegemea mahitaji ya ndani.
“Upatikanaji wa bidhaa za afya umeongezeka kutoka asilimia 51 Juni 2022 hadi kufikia asilimia 64 Juni 2023, lakini pia upatikanaji wa dawa umefikia asilimia 81, Juni 2023 kutoka asilimia 57 Juni 2022”
Pia alisema wamefanikiwa kuongeza idadi ya mikataba ya muda mrefu kutoka mikataba 100 yenye bidhaa za afya 711 kwa mwaka wa fedha 2021/22 hadi kufikia mikataba 233 yenye bidhaa 2,209 kwa mwaka wa fedha 2022/23
Tukai alisema miradi mbalimbali imetekelezwa ikiwemo mradi wa UVIKO-19 unaohusu hospitali na vituo vingine vya kutolea huduma za afya ikiwemo hospitali za rufaa za mkoa ya Kigoma , Kagera, Lindi, Katavi na Lugalo ambapo gharama za mradi kwa upande wa thamani ya vifaa vilivyotarajiwa kusambaza ni Bilioni 17.17 huku thamani ya vifaa vilivyosambazwa ikiwa ni shilingi Bilioni 17.62 sawa na asilimia 102 za utekelezaji.
Kwa upande wa uzalishaji wa bidhaa za afya, Tukai alisema MSD imefanikiwa kukamilisha ujenzi wa kiwanda Cha mipira ya mikono (Gloves) kilichopo Njombe, kuhusisha Sekta Binafsi kwa kutambua maeneo ya uwekezaji ya bidhaa za afya za kimkakati za vidonge, rangi mbili, vimiminika n.k na bidhaa zitokanazo na zao la pamba.
Aliongeza kuwa “Tumefanikiwa kukamilisha taratibu za usajili na uendeshaji wa kiwanda Cha barakoa Cha N95 kilichopo keko ambacho uzalishaji wake utakidhi mahitaji ya barakoa nchini
More Stories
Maandamano ya kuunga mkono Samia, Mwinyi yatikisa Tabora
Haya hapa matokeo yote kabisa ya Form Four
Kisarawe kukata keki Birthday ya Rais Samia