January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Msanii Mkongwe Saidi Mabera afariki dunia

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

MWANAMUZIKI mkongwe katika muziki wa dansi na mbobezi kwenye kupiga gitaa la solo kwenye bendi ya Msondo Ngoma, Said Mabera amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.

Akizungumza na TimesMajira Online kwa njia ya simu, meneja wa bendi ya Msondo Ngoma Said Kibiriti, amethibitisha taarifa hiyo na kusema kuwa Mabera aliaga dunia majira ya saa 6 kasoro usiku wa kuamkia leo.

Hata hivyo, kwa mujibu wa Kibiriti, marehemu Mabera alisimama kufanya shughuli zake za muziki takribani miezi miwili iliyopita kutokana na Afya yake kutrokuwa nzuri mpaka umauti unamfika, hivyo anatarajiwa kuzikwa leo saa 10 jioni nyumbani kwake Mbezi mwisho.

%%%%%%%%%%