January 5, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Msalala kuokoa mil. 20/- kwa kuamua kutumia vishkwambi

Na Patrick Mabula,TimesMajira Online. Kahama

HALMASHAURI ya Msalala wilayani Kahama, itaokoa zaidi ya sh. milioni 20 kwa mwaka baada ya kuamua kutumia teknolojia ya tablet (vishkwambi) kutokana na kuodokana na matumizi ya karatasi, kuchapa nyaraka na kuwasambazia makashabrasha madiwani na wataalamu badala yake watatumia mfumo huo.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala, Simon Berege baada ya madiwani kuapishwa kisha kuwagawia vishkwambi madiwani wote 28 na wataalamu 18 watakaopewa baadaye zikiwa na thamani ya sh. milioni 20 na zitaunganishwa katika grupu moja na zitatumika kuwatumia ajenda za vikao, badala ya kuchapa makashabrasha na kuwasambazia.

Berege amesema matumizi ya teknolojia hiyo, itaokoa zaidi ya sh. milioni 200 kwa mwaka zilizokuwa zikitumika kununua karatasi na kazi ya kuchapa makashabrasha na kisha kuwasambazia madiwani kwenye kata zao lakini kwa matumizi ya vishikwambi kwa wataalamu na madiwani, watakuwa wanafanya majadiliano kwa teknolojia hiyo.

Naye Katibu Tawala Wilaya ya Kahama, Thimos Ndanya amepongeza utaratibu huo alipokuwa akigawa vishkwambi hivyo, ambapo aliwataka madiwani kuvitunza na kuzitumia kwa malengo yaliyokusudiwa kwa sababu vinawasaidia kuokoa fedha na muda wa kusafiri kila mara kwenda halmashauri.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Msalala, Idd Kassim amewataka madiwani kuwa wamoja na mshikamano na kuwatumia vizuri watendaji katika kuwatumikia wananchi changamoto zao mbalimbali, kutakuwa na mafanikio kwenye suala la maendeleo.

“Mimi kama mbunge nipo pamoja nanyi ndugu zangu madiwani, sitampendelea mtu yeyote kila mmoja twende tukawajibike kwa wananchi kwa mafanikio na tukawasimamie viongozi wenzetu waliopo chini yake kuanzia Mwenyeviti wa Vitongoji, Vijiji na isiwe kila jambo anatafutwa mbunge pekee,” amesema Kassim.