Na Mwandishi wetu,Timesmajira
Msajili wa Hazina,Nehemiah Mchechu, amewataka watumishi wa ofisi yake kuutumia mwezi mtukufu wa Ramadhani kama nyenzo ya kufanya kazi kwa bidii na maarifa makubwa kwa faida ya Taifa la Tanzania.
Mchechu aliyasema hayo Jumatatu, Machi 24, 2025 wakati wa hafla ya iftar iliyofanyika katika ukumbi wa hoteli ya KingJada, Morocco Square, Dar es Salaam kwa watumishi wa ofisi ya Msajili wa Hazina iliyoandaliwa na Msajili wa Hazina mwenyewe.

“Mwezi huu unatufundisha uvumilivu, kujitolea, na huruma kwa wengine, maadili ambayo pia yana nafasi muhimu katika mazingira ya kazi.
“Natumai kila mmoja wetu ataendelea kuyaishi haya mafunzo hata baada ya mwezi huu kumalizika,”amesema
Mchechu ameelezea kutambua na kuthamini mchango wa kila mtumishi katika mafanikio ya OMH, na kusema kuwa ni matarajio yake kuwa roho ya mshikamano itaendelea hata baada ya Ramadhani.

Amesema lengo la kuwaleta pamoja watumishi ili wapate Iftari si tu ni kuvunja funga, bali pia kuimarisha mshikamano wa watumishi kama familia moja ya Ofisi ya Msajili wa Hazina.
“Ni furaha kubwa kuwa pamoja nanyi katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani, mwezi wa rehema, msamaha na baraka nyingi.” Amesema Mchechu.
Ametoa wito kwa watumishi kuwaombea wenzao walioko mbali, jamii za Tanzania, na taifa kwa ujumla, ili waendelee kuishi kwa amani, afya njema, na mafanikio.
More Stories
Prof.Muhongo apongezwa kuleta majadiliano sekta ya elimu Musoma
Ntiboneka:Mashirika wekezeni katika kubadilisha fikra za vijana,wanawake
Simbachawene:Watendaji wakuu acheni kuwaona wakaguzi wa ndani kama maadui