November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mradi Wazinduliwa kuinua Uchumi wa Buluu

Na Iddy Lugendo, TimesMajira Online

IMEELEZWA kuwa bado kunahitajika ushirikishwaji wa sekta binafsi katika kuinua uchumi wa buluu ambao unategemea Bahari.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam Wakati wa kufungua mradi wa uchumi wa bluu katika nchi za kusini Maghalibi, mwakilishi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Miriam Kabaka, alisema Mradi huo umeandaliwa na shirika lisilo la Kiserikali la WWF.

Kabaka alisema licha ya nchi kubarikiwa Bahari, Maziwa na mito bado uchumi wa bluu ambao unaonekana upo chini, hivyo jitihada zinahitajika kwa sekta binafsi katika kutoa elimu ya kupiga vita uvuvi haramu pamoja na kuhamasisha nchi kuwa na sera ya kutambua uchumi wa buluu.

Aidha, Kabaka amesema Mradi huo umekuja kipindi muhimu na unatazamiwa kuja na matokeo chanya katika uchumi wa bluu na kuzifanya taasisi za fedha kuweza kuwakopesha wavuvi ili kuinua uchumi.

Hivyo, Kabaka alitoa shukrani kwa Taasisi ya WWF kutafuta fedha kwa ajili ya mradi huo na kushirikiana na serikali katika kuinua uchumi wa bluu.

Kwa upande wake Sevelin Kalonga ambaye ni mfanyakzi wa shirika la uhifadhi wa mazingira duniani WWF, ofisi ya Tanzania amesema kuwa mradi huo kwa upande wa Tanzania utakua ni wa Taia zima ambapo utaangalia sehemu za ukanda wa maji huku akikisitiza ushikirishwaji wa wadau ili upatikane mpango mkakati ambao ni jumuishi na usiishie kwenye bahari pekee.

Pia alisema sehemu zenye ukanda wa maji ikiwemo Dar es salaam, Rufiji, Kilwa,na shemu nyinginezo watakua ni wadau muhimu na walengwa katika kutoa takwimu nza kutosha kwa lengo la kuwa na mazingira wezeshi ya kutekeleza uchumi wa bluu Nchini Tanzania.

Aliongeza kuwa mwishoni mwa mradi huo wanatarajia kua na mpango mkakati wa uchumi wa bluu wa Tanzania ambapo matarajio yatajumuisha ukanda wa bahari na sehemu zote zenye vyanzo vya maji, huku akibainisha kuwa dhana ya uchumi wa bluu ni pana na ina mambo mengi.