January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mradi wa bwawa la Julius Nyerere waendelea kwa Kasi kubwa

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Ndani ya msimu mmoja wiki iliyopita Wizara ya Nishati imefanikiwa kujaza maji kwa kiwango kinachotosheleza kuzalisha umeme kwenye bwawa la Julius Nyerere.

Kina Cha bwawa lolote lile ni mita 184 kutoka usawa wa Bahari, kina kinachotakiwa kufikiwa ili uanze kuzalisha umeme ni mita 163 kutoka usawa wa Bahari na siku ya Jana imefikia mita 163.61.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nishati January Makamba wakati akizungumza na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam ambapo amesema hadi sasa mradi wa kufua umeme rufiji Julius Nyerere unaendelea kwa Kasi kubwa na sasahivi umefikia asilimia 89 huku hadi kufikia mwezi Julai mradi huo utafikia asilimia 90.

“Huko nyuma kumekuwa na hofu kubwa ya je maji yatajaa kuweza kuzalisha umeme katika bwawa hilo, tulikadiria tutakuwa na misimu mitatu ambayo ndiyo itatosheleza kujaza bwawa hilo lakini ndani ya msimu mmoja wiki iliyopita Wizara ya Nishati imefanikiwa kujaza maji kwa kiwango kiachotosheleza kuzalisha umeme kwenye bwawa la Julius Nyerere”

Makamba amesema Kina Cha bwawa lote la Nyerere ni mita 184 kutoka usawa wa Bahari, kina kinachotakiwa kufikiwa ili uanze kuzalisha umeme ni mita 163 kutoka usawa wa Bahari na Hadi kufikia siku ya Juzi wamefikia mita 163.61.

Aidha Makamba amesema kazi ya ufungaji mitambo inaendelea na mnamo mwezi wa pili wataanza kufanya majaribio ya kuzungusha mitambo kwa maji.

“Imani yetu ni kwamba mwezi wa 6 mwakani tutaanza kutoa umeme pale Julius Nyerere na kuingiza umeme wa kwanza kwenye gridi ya Taifa”

Kuhusu Ujazo wa bwawa la Julius Nyerere Makamba amesema ujazo ni mita za ujazo Bilioni 30 Hadi kufikia Juzi maji yaliyoingia mule ndani ni mita za ujazo Bilioni 13. 8 ambao ni sawa na asilimia 43.