January 9, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mradi wa BRT hautoligusa Sanamu la Askari Posta

Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online. Dar

WAKALA wa Barabara Tanzania ( TANROADS), imewaondoa hofu wananchi kuhusiana na taharuki iliyozuka mapema wiki hii, kuhusu kuondolewa kwa Sanamu ya Askari, (Askari Monument) ya Jijini Dar es salaam kutokana na ujenzi na uboreshwaji wa barabara unaendelea katika baadhi ya maeneo Jijini humo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Mawasiliano (TANROADS), imeelezwa kuwa, ujenzi unaendelea katika mradi wa BRT awamu hii ya tatu, hautaondoa wala kugusa Sanamu hiyo ya Askari, iliyopo katika makutano ya Mtaa wa Azikiwe na Samora.

Aidha imeelezwa kuwa, kutokana na ufinyu wa eneo la barabara katika makutano hayo, duara la bustani linalozunguka Sanamu hiyo, litapunguzwa bila kuathiri hadhi ya Sanamu na usalama wa matumizi ya barabara.