November 16, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mradi wa Amref, Serikali wazaa matunda

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Mradi wa mawasiliano ya mabadiliko ya tabia afya HBCC II umefanikiwa Kuboresha Miundombinu ya Maji safi ikiwa ni kuongeza mtandao wa maji, kujenga Minara minne (4) ya tank za Maji ya akiba yenye ujazo wa liter 8,000 kwenye Zahanati ya Mpamaa, Chididimo, Kikombo na Makole.

Mradi huo Mradi huo ulioanza kutekelezwa tarehe 1/7/2022 (Miezi 3 baada ya kusainiwa) katika mikoa ya Mwanza na Dodoma unaotegemewa kuisha tarehe 31/03/2023 uliotekelezwa na shirika la Amref Health Africa Tanzania, kwa kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania, kupitia Wizara ya Afya, Kigezo kikubwa cha mafanikio ni Ushikiri wa Wadau wote (Serikali, Vyombo vya Habari, na wana-Jamii), tangu mwanzo wa Mradi, na wakati wa utekelezaji.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Amref Health Africa Tanzania Ndg. Mtengela Hanga, alisema Mradi umetekelezwa kwa mafanikio makubwa kwenye Kata 31 katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, na kwenye Kata 30 katika Halmashauri ya Jiji la Ilemela – Mwanza.

“Mradi huo pia umesaidia kujenga vituo 20 vya Kunawia Mikono kwenye shule za Msingi, Zahanati na Masoko.”

Pia alisema mradi huo umesaidia Kugawa vinawia mikono vya kisasa aina ya SATO 5,000 (Dodoma pekee), vyenye gharama ya TSH 35,012,000. Lengo ni kuhamasisha jamii kuwa na tabia ya kunawa mikono mara kwa mara.

Dkt. Hanga alisema Amref Tanzania imeendelea kushirikiana na Serikali hususani Wizara ya Afya na TAMISEMI katika kuboresha sera za afya kwa ujumla wake ambapo kupitia mradi huo Watu 60,053 wamefikiwa moja-kwa-moja na ujumbe kupitia Maafisa afya 41, na Wahudumu wa Afya 123 katika ngazi ya jamii waliopata mafunzo ya namna ya kuhamasisha unawaji wa mikono na utayari wa kupokea Chanjo ya UVIKO-19 kwenye ngazi ya jamii.

Amref imewafikia watanzania wengi kupitia miradi ya afya kwa afua mbalimbali inayotekelezwa katika mikoa mbalimbali ya Tanzania ambapo kupitia mradi huo, wamefanikiwa kukabidhi vifaa vya usafi wa mazingira na kinga ya mwili (PPEs), vyenye thamani ya Tsh Tsh 24,496,800 kwa Mkoa wa Dodoma na Mwanza.

“Shirika la Amref Health Africa Tanzania linachukuwa fursa hii kuwapongeza na kuwashukuru Wadau, hasa Jamii kwa kuonesha ushirikiano na hamasa kubwa wakati wa utekelezaji wa mradi. Hii ni pamoja na kupokea mafunzo, kujitokeza kwa wingi kuchanja dhidi ya Uviko-19 na kubadili tabia inayolenga kupunguza maambukizi ya magonjwa yatokanayo na uchafu, hasa kunawa mikono kwa maji safi na sabuni.” Alisema Dkt. Hanga

Dkt. Hanga alisema Pamoja na Shirika la Amref Health Africa Tanzania kuamua kujenga miundo-mbinu isiyohamishika ili kuepukana na changamoto za wizi wa vifaa vya kunawia mikono aliwaomba watumiaji, wananchi na Mamlaka husika kuweka mkakati madhubuti wa kulinda miundo-mbinu hiyo.

Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Amref Health Africa Tanzania Ndg. Mtengela Hanga (kushoto) akikabidhi baadhi ya vifaa vya usafi na kinga mwili kwa mkuu wa wilaya ya Dodoma Mhe. Jabir Shekimweri (katikati) wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika jijini Dodoma.
Vifaa hivyo vitakavyotumiwa na wananchi pamoja na taasisi mbalimbali za afya vimetolewa kupitia mradi wa Mawasiliano ya Mabadiliko Tabia na Afya unaotekelezwa katika jiji la Dodoma na Mwanza.