Stephen Noel,Timemajira Online. Mpwapwa
WANANCHI wilayani hapa wameiomba serikali, kuwajengea madaraja yaliyobomoka miaka miwili iliyopita kwa kusombwa na maji, ili kuungunisha mji huo ambao kwa sasa ni daraja moja pekee linalotumika ambalo nalo halina usalama wa kutosha.
Sambamba na hilo, pia wameishukuru serikali kwa kuwajengea daraja lijulikanlo kama kwa Mkuu wa Wilaya lilokuwa limebomoka kutokana na kusombwa na mvua mwaka 2019 na kusababisha adha wa wananchi wa mjini hapa.
Pia wameiomba serikali kuweza kujenga daraja la Tanesco, ambalo nalo lilisombwa kutokana na mvua nyingi kunyesha mwaka 2019.
Akizungumza na Majira mmoja wa wananchi wa mji huo, Gidion Lesilwa amesema tangu kubomoka kwa madaraja hayo, kumesabaisha adha kubwa na kusabaisha hali ya maisha kupanda.
Lusilwa amesema anaishukuru serikali kwa kuona juhudi zilizofanywa na kuanza kujengwa kwa daraja la Miembeni lijulikalo kama daraja la kwa Mkuu wa Wilaya ambapo kwa sasa liko hatua za mwisho.
Amesema daraja hilo likikamilika, litafungua mawasiliano kati ya wakazi wa Mtaa wa Mjini na Igovu pamoja na National Housing, ambao kwa sasa huwalazimu kuzunguka kupitia daraja la NMB ambalo nalo halina uimara wa kutosha.
Mkazi huyo amesema kutokana na madaraja ya mto huo kusombwa yote kwa sasa linatumika daraja moja ambalo linazidiwa na msongamano na hivyo kusabaisha ajali kwa watembea kwa miguu mara kwa mra, hasa wanafunzi.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Vighawe, Dickson Mahuwi amesema daraja la Tanesco ambalo lilikuwa kiungo kati ya Kata ya Ving’hawe na Mpwapwa mjini ambalo lilisombwa na maji miaka miwili iliyopita na hivyo kuendelea kusabaisha adha kwa wananchi wake.
Amedai Kamati ya Ulinzi na Usalama, inalifahamu suala hilo na walishawasiliana na uongozi wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Dodoma kwa hatua zaidi, ambazo zimekuwa kimya kwa zaidi ya miaka miwili sasa.
Mahuwi ameuomba uongozi wa wilaya, kuunganisha nguvu kwa uongozi wa TANROADS Mkoa ili kuweza kukamilisha kwa daraja hilo ambalo linahudumia zaidi ya wakazi 9,000 wa kata zaidi ya nne za Vigahwe, Kimagai, Godegode na Pwaga.
Akizungumzia hali hiyo Mhandisi anayejenga daraja la Miembeni, amesema wanatarajia kukamili kazi hiyo mwishoni mwa mwezi huu na kwa sasa wamefikia asilimia 75 ya ujenzi wote hadi kukamilika kwake ambalo litatumia sh. 972,370,287.50.
More Stories
CCM hakuna kulala, Nchimbi atua Tabora kwa ziara ya siku mbili
Kongamano la Uwekezaji na Biashara lafunguliwa Pwani
Rais Samia afurahia usimamizi mzuri wa miradi