December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mpoto awataka watanzania kuipenda, kuiheshimu lugha ya kiswahili

Na Jackline Martin , TimesMajira Online

Imeelezwa kuwa kiswahili ni moja ya lugha iliyo enea katika Mataifa ya Afrika kutokana na jitihada mbalimbali zilizo fanyika katika kukuza lugha hiyo.

Hayo yamesemwa na Msanii wa muziki wa Asili, Mrisho Mpoto wakati alipotembelea Banda la Wizara ya Utamaduni , Sanaa na Michezo katika maonesho ya 48 ya biashara ya kimataifa sabasaba.

Kutokana na hivyo Mpoto amewataka watanzania kuwa na utamaduni wa Watanzania kuipenda na kuiheshimu lugha ya kiswahili kwa kuzungumza.

“Tusipoiheshimu lugha yetu ya kiswahili hakuna mtu mwingine anaweza kuiheshimu lugha hii, lugha hii sasahivi imeingia kwenye nyanja za kimataifa ambapo UN na Dunia kupitia UNESCO wameitambua na hivyo kwa sasa Dunia nzima imeamua kuzungumza lugha ya kiswahili”

Mpoto amesena Licha ya makabila 120 na lugha ndogondogo 64 bado wote wanaunganishwa na lugha Moja ya kiswahili.

“Watanzania tuiheshimu lugha yetu kwasababu kiswahili ni bidhaa na biashara, ukiacha ni lugha ya Mawasiliano hivyo twendeni tukaiuze na tukaitumie na kuwaambia watanzania licha ya makabila 120 na lugha ndogondogo 64 lakini wote tunaunganishwa na lugha Moja ya kiswahili” Amesema

Mbali na hayo, amewataka wananchi kwenda kutembelea maonesho hayo ili kujionea na kupata fursa mbalimbali