Na Patrick Mabula , Mbogwe.
Wabunge Luhanga Mpina wa Kisesa na Nicodemas Maganga wa Mbongwe wamesema watandelea kuwafichua wale viongozi wasiokuwa waaminifu,wabadhilifu na mafisadi licha ya kuwa wamekuwa wakikimbilia kwenye chama chao cha CCM kwa lengo la kuyaficha mabaya wanayoyafanya.
Wabunge hao wameeleza hayo juzi kwenye mkutano wa hadhala uliofanyika jimbo la Mbogwe katika mji mdogo wa Masumbe na ambapo walisema wataendelea kuwashughulikia wabadhilifu licha wamekuwa wakikimbilia kwenye chama kushitaki ili kulinda ubadhilifu wanaofanya.
Akiongea katika mkutano huo mbunge wa Kisesa , Mpina amesema ataendelea kuwafichua na kupambana na viongozi wala rushwa , wabadhilifu na hataogopa kwa maslahi ya umma, pamoja na kuwa anapowafichuwa wanakwenda ndani ya chama chake cha CCM kumshitaki na kumsema kuwa mpizani.

Amesema fedha za umma zimekuwa zikiliwa na baadhi ya viongozi wachache wasiokuwa waaminifu waliopewa dhamana ya uongozi kwa hilo nitaendelea kupambana nao pamoja na kuwa wamekuwa wakikimbilia CCM kunishitaki kwa lengo kuficha madhambi yao.
Mpina katika mkutano huo alichukua katiba ya CCM na kuanza kunukuu baadhi ya vifungu na kuanza kuwasomea wananchi katika mkutano huo na kusema “ katiba ya chama inakataa rushwa , wizi , ubadhilifu “ kwa hiyo ataendelea kuwashughulikia kwa mjibu wa katiba hiyo.

Naye mbunge wa jimbo la Bongwe , Maganga amesema wilaya ya Mbogwe imepiga hatua kubwa katika suala la miradi ya maendeleo kwenye sekta zote kuanzia elimu , maji , kwa kutokana na kuzisimamia vizuri fedha za umma na kudhibiti ubadhilifu.

Maganga amesema kwa miaka minne ya Ubunge wake Serikali imeweza kupeleza jimboni kwake zaidi ya sh.74 bilioni za miradi mbalimbali ya maendeleo na kuhakikisha na zimefanya vizuri na kutoa salamu zake na za wapiga kura wake kwa kutoa shukuru kwa mheshimiwa Rais Dkt .Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anayofanya.
Kwa upende wao baadhi ya wananchi wa jimbo la Mbogwe Daud Mashishanga ambae ni Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Shinyanga A, Masumbwe na Paulo Kingi wa Kijiji cha Nyakafulu wamesema wanampongeza Mbunge wao na Rais Samia kwa kazi nzuri wanazofanya katika kuwaletea maendeleo .
More Stories
TMDA yajivunia kuanzisha mfumo thabiti wa udhibiti wa vifaa tiba na vitendanishi
Kikwete kuungana na marais watatu kushiriki Kongamano la nane la viongozi Afrika
Katavi yazindua kampeni kukabiliana na udumavu