Na Judith Ferdinand, Mwanza
Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza (MPC) kwa kutambua umuhimu wa wanahabari katika kuchochea maendeleo ya taifa, imezindua tuzo ya heshima kwa wanahabari shujaa.
Ambapo katika kusherekea siku ya kimataifa ya wanawake dunia ambayo uadhimishwa kila ifikapo Machi 8 ya kila mwaka,MPC imetumia siku hiyo kuwapatia tuzo hizo kwa mwaka 2022, wanahabari wanawake waliopoteza maisha Januari 11 mwaka huu kwa ajali ya gari ambao ni Husna Mlanzi na Johari Shani,ikiwa ni sehemu ya kutambua na kuthamini mchango wao katika ujenzi wa taifa kupitia taaluma yao ya uandishi wa habari.
Zoezi hilo limefanyika kwenye hafla fupi iliyoandaliwa na MPC kwa ajili ya kuwapongeza waandishi wa Habari wanawake wa Mkoa wa Mwanza.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa tuzo hizo ulionda sambamba na kuadhimisha siku ya kimataifa ya wanawake dunia,Mwenyekiti wa MPC Edwin Soko,amesema utoaji wa tuzo hizo kuanzia mwaka 2023 na kuendelea zitatolewa kila ifikapo Januari 11.
Hiyo ikiwa ni siku ya kumbukumbu ya vifo vya waandishi wa habari watano waliofariki wilayani Busega, Mkoani Simiyu kwa ajali ya gari walipokuwa wakienda kutimiza majukumu yao ya kikazi wilayani Ukerewe.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya Desk & Chair Foundation Alhaj Sibatin Meghjee, akizungumza wakati akizindua tuzi hizo amewapongeza waandishi wa habari wanawake wa Mkoa wa Mwanza kwa kufanya kazi zao kwa weledi na kuwaomba wazidi kuzingatia maadili ya uandishi wa habari.
Mmoja wa waandishi wa habari wanawake Mkoa wa Mwanza Clara Matimo alitoa ombi maalumu kwa mgeni rasmi kwenye kuwashika mkono waandishi wanawake kwenye kusudio lao la kuwa na mradi wa bajiji kwa ajili ya kuongeza kipato kwa waandishi wa habari.
Meghjee alifanya zoezi la kukabidhi vyeti vya tuzo ya heshima ya mwanahabari shujaa mwaka 2022 kwa ndugu wa familia ya marehemu Husna Milanzi na Katibu wa MPC Blandina Aristide aliyepokea kwa niaba ya familia ya Johari Shani, ambao wote walipoteza maisha kwenye ajali ya Januari 11, 2022
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi