Na Judith Ferdinand, TimesMajira Online Mwanza
Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Mwanza MPC imeendesha mdahalo wa ulinzi na usalama wa mwandishi wa habari awamu ya tatu.
Ambapo lengo la mdahalo huo ni kufanya kazi kwa kushirikishana kati ya Jeshi la Polisi na Waandishi wa Habari.
Mdahalo huo umeandaliwa na MPC chini ya ufadhili wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa habari Tanzania (UTPC) ikishirikaiana na Shirika la International Media support (IMS).
Akizungumza wakati akifungua mdahalo huo kwa niaba ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Ramadhan Ng’azi,Mrakibu wa Jeshi la Polisi Mkoani hapa SP. Denis Rwiza ameeleza kuwa kuwepo kwa mdahalo huo ni moja ya nia njema katika maisha ya polisi na waandishi wa habari.
Ameeleza kuwa wote wanafanya kazi kwa mujibu wa sheria, hivyo kila mmoja anawajibu wa kulinda haki ya kila mmoja kiutendaji bila kuathiri upande wowote.
Pia amewasihi Waandishi wa habari na Askari Polisi Mkoani hapa kufanya kazi kwa kushirikiana huku wakiweka maslahi ya taifa mbele.


More Stories
TAMWA yakumbusha jamii kupinga ukatili wa kijinsia kuelekea siku ta wanawake Duniani
Wanawake washauriwa kuchangamkia fursa za uchumi
Aida:Wanawake wakipata haki zote itapunguza migogoro