November 16, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mpango kazi kuhusu wanawake, amani na Usalama wajadiliwa

Na Jackline Martin, TimesMajira Online

The Mwalimu nyerere Foundation kwa kushirikiana na UN Women na Wizara ya maendeleo ya jamii jinsia wanawake na makundi maalum wamepanga kuja na mpango kazi wa Taifa kuhusu wanawake, amani na usalama.

Akizungumza wakati wa majadiliano hayo yaliyowakutanisha na wadau mbalimbali wa maendeleo wakiwemo, wanafunzi, vijana, CSOs n.k, yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam, Afisa msimamizi utawala na fedha kutoka The Mwalimu Nyerere Foundation, Erica Kiduko amesema lengo la mpango mkakati huo ni kupata maoni mbalimbali ili waweze kuandaa mpango mkakati huo utakaoenda kumlinda Mwanamke, mtoto na msichana pale anapopata madhara.

“Unaumuhimu kwasababu tunaangalia ni jinsi gani ya kumlinda Mwanamke, mtoto, msichana na endapo Mwanamke anapopata madhira tofauti tofauti kama kubakwa, unyanyasaji wa kijinsia je ni haki gani za kumpatia ahueni”

Aidha Kiduko amesema Mpango huo ni endelevu, hivyo aliwataka wadau mbalimbali kujitokeza kwa wingi kwani Kwa sasa wapo Bara kwaajili ya kukusanya maoni hayo lakini pia wataenda sehemu tofautitofauti ikiwemo Zanzibar.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Global Peace Foundation Tanzania, Martha Nghambi amesema mkutano huo ni mkubwa na ni wa umuhimu kwani utaweza kuweka muelekeo na mwangaza wa jinsi gani wanaweza wakatekeleza kikamilifu yale ambayo wameyapanga kuweza kuyatekeleza katika maeneo mbalimbali.

Aidha Nghambi amesema tangu kuanza kwa mpango mkakati kama huo hadi sasa kumekuwa na matokeo chanya ndiyo maana wamewiwa kuendeleza na kuja na mpango mkakati huo wa Taifa kwaajili ya wanawake, amani na usalama.

“Matokeo chanya yamepatikana kwa ngazi ya awali had sasa tulipofikia, lakini pia tumefanikiwa kufanya uchunguzi kujua kuna mapungufu gani na matatizo yaliyopo kwenye ripoti ili tuweze kuyatatua na kuweza kufika pale tulipofika”

Mwanafunzi kutoka chuo cha diplomasia, Steven Isdori amesema wao kama vijana wana kilasababu kubwa ya kuchangia na kushiriki kwasababu vijana ndiyo nguvu kazi ya Taifa, kwani ukimuelimisha kijana ni kulielimisha Taifa na kizazi kijacho.

Pia amesema Wanawake duniani kote wamekuwa wakisumbuliwa na matatizo mbalimbali, haki zao zimekua zikiminywa na watu tofauti tofauti hivyo aliwashukuru Mwalimu nyerere Foundation kupitia serikali kwa kuja na mpango madhubuti kwaajili ya kupata suluhisho la namna gani wanaweza kuwafanya wanawake wawe katika kundi linalotambulika zaidi kwenye jamii.

Afisa msimamizi utawala na fedha kutoka The Mwalimu Nyerere Foundation, Erica Kiduko akizungumza na waandishi wa habari leo wakati wa majadiliano yaliyowakutanisha wadau mbalimbali wa maendeleo wakiwemo, wanafunzi, vijana, CSOs n.k, yenye lengo la kukusanya maoni ili waweze kutoa mpango kazi wa Taifa kuhusu wanawake, amani na usalama. Mkutano huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam, katika ukumbi wa mikutano wa Four Points by Sheraton .
Mkurugenzi wa Shirika la Global Peace Foundation Tanzania, Martha Nghambi akizungumza na waandishi wa habari leo wakati wa majadiliano yaliyowakutanisha wadau mbalimbali wa maendeleo wakiwemo, wanafunzi, vijana, CSOs n.k, yenye lengo la kukusanya maoni ili waweze kutoa mpango kazi wa Taifa kuhusu wanawake, amani na usalama. Mkutano huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam, katika ukumbi wa mikutano wa Four Points by Sheraton .
Baadhi ya wadau mbalimbali wa maendeleo wakifuatilia majadiliano yenye lengo la kukusanya maoni ili waweze kutoa mpango kazi wa Taifa kuhusu wanawake, amani na usalama. Mkutano huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam, katika ukumbi wa mikutano wa Four Points by Sheraton .