December 27, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Motto aunga mkono Juhudi za Rais Dkt. Samia

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Mjumbe kamati ya siasa kata ya Buyuni Jessica motto ameishukuru serikali pamoja na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Samia suluhu Hassan kwa kuwapatia kiongozi mwenye kuchapa kazi na kutatua changamoto za wananchi wake.

Dotto ambaye pia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya kigezi Strong Woman, ni mshiriki mkubwa katika maswala ya kijamii kama kupinga ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto kwa kushirikiana na wizara ya maendeleo ya jamii jinsia na makundi maalum chini ya waziri mwenye Dhamana hiyo Doroth Gwajima.

Jessica motto ni mpambanaji kweli kweli katika kata Yao ya chanika iliyoko ukonga chini ya Mbunge Jerry Slaa ambaye anajihusisha na kushiriki maendeleo ya Jimbo pamoja na kushiriki katika kutoa elimu kwa wananchi wa Jimbo hilo kuhusu maendeleo yanayofanywa na Rais Dkt. Samia.

Motto amekuwa msaada mkubwa sana kwa jamii ya watanzania wote bila kuangalia Chama au dini.

Kadhalika Dotto amekuwa mstari wa mbele katika kusimamia miradi ya maendeleo katika kata hiyo ya chanika na kuandaa majukwaa ya wanawake katika Kata ya Chanika.

Mbali na hayo, Dotto amekuwa akimuunga mkono Rais Dkt. Samia katika kumkomboa mwanamke na kumtoa kuwa tegemezi na kwenda kujiajiri kupitia Kigezi Woman.

Motto amekuwa msaada kwa viongozi wa ngazi za Kata, Wilaya, Vijiji na vijana wa Chama cha Mapinduzi wa Kata za Buyuni na Pugu Mkuranga.