Na Irene Clemence, TimesMajira Online
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Bara John Mongela amewahaidi wananchi na wanachama wa CCM kuwa atahakikisha Utendaji ndani ya Chama na utumishi unahakisi ukubwa wa chama hicho.
Mongela ametoa kauli hiyo jijini Dar es salaam leo April 5 , 2024 wakati wa mapokezi ya viongozi wa sekretarieti ya Chama hicho katika ngazi mbalimbali ikiwemo katibu wa itikadi uenezi na Mafunzo,katibu mkuu UVCCM na katibu mkuu wa Jumuiya ya wazazi.
” Ninawahidi nitawajibika kwa kadri Mwenyezi Mungu atakavonijalia kuhakikisha Utendaji ndani ya Chama na utumishi una hakisi ukubwa wa chama chetu”amesema Mongela
Mongela amesema uteuzi uliofanya na mwenyekiti wa chama hiko ambae pia ni Rais wa Jamuhuri ya Muungano Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa viongozi hao ndani ya chama unaonyesha taswira halisi ya uongozi wake na utendaji wake.
Aidha amesema Jumuiya zote za Ccm zimeimarishwa vizuri na kujipanga katika uchaguzi wa serikali za mtaa na serikali kuu.
Pia alitoa rai kwa vijana kutokukubali kutishwa kwani chama kipo imara hivyo wakilinde na kukitetea.
“Hii safu ni ujumbe tosha kama kuna mtu alikua hamjui Rais Samia kwa safu hii lazima watamuelewa chama hakina hakina namna nyingine zaidi ya kusimamia maendeleo ya nchi na kwa kasi yake ya kutatua changamoto za wananchi basi inatosha kuonyesha utendaji wake uliotukuka”amesema Mongela
Awali Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM, Jokate Mwegelo amesema uteuzi alioupata umempa fursa ya kuweka historia ndani ya Jumuiya kwa kuwa mwanamke wa kwanza mtendaji katika Jumuiya hiyo.
Amesema atahakikisha vijana wanakuwa imara na kukilinda na kukitetea chama popote.
“Tutatafuta na kuzilinda kura kwa ulinzi imara na sisi kama vijana hatutakaa nyuma tutashiriki pia kugombea katika nafasi mbalimbali za uongozi kuanzia ngazi ya serikali ya mtaa mpaka serikali kuu”,amesema Jokate
Naye,Katibu Mkuu wa Umoja wa wazazi Tanzania Ally Hapi amesema utayari wake katika kuitumikia nchi na chama hauna mashaka hivyo ameahidi kushirikiana na wengine katika kuhakikisha wanakiletea ushindi chama cha Mapinduzi CCM.
“Niwahaidi Jumuiya ya wazazi tutakwenda kufanya kazi usiku na mchana kuhakikisha tunaijenga upya jumuiya yetu lakini pia tupo tayari kwa mapambano niwape salam upinzani wasitegemee huruma uchanguzi ni kazi twende kwa wananchi tukatafute kura”,amesema Hapi.
Hata Hivyo Katibu wa Halmashauri kuu ya Ccm Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Amosi Makala amesema yupo tayari na amejipanga vizuri kuhakikisha anakijenga chama huku akitoa rai kwa wapinzani kufanya siasa za hoja na yupo tayari kujibu hoja na si vioja.
Nao Vongozi wa Umoja wa bodaboda na bajaji pamoja na viongozi wa Machinga mkoa wa Dar es salaam wamepongeza uteuzi wa wagombea hao huku wakiamani utaenda kuendeleza umoja uliokuwepo na kuwaunganisha.
Kikao cha Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi chini ya mwenyekiti wake Rais Dk Samia Suluhu Hassan kiliwateua watendaji hao ndani ya chama ili kuhakikisha wanawatumikia chama chao na kuhakikisha wanashinda kwa kishindo katika chaguzi zijazo.
More Stories
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa
NLD kipo tayari kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa