March 18, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

MNH yapokea msaada wa taulo za matiti 2400 kutoka kampuni ya Ackijal

Na Mwandishi wetu, Timesmajira

Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imepokea msaada wa taulo za matiti (breast pads) 2,400 zenye thamani ya TZS 5 Mil. kutoka Ackijai Company Limited kwa ajili ya kusaidia akina mama mara baada ya kujifungua.

Msaada huu unalenga kuwanufaisha hasa akina mama wanaojifungua na kuendelea kuwa chini ya uangalizi maalum hospitalini pamoja na watoto wao, hususan wale wanaopata matatizo ya kiafya baada ya kujifungua ambapo katika kipindi hiki, mama anapaswa kuendelea kunyonyesha ili kuhakikisha mtoto anapata lishe bora, lakini uvujaji wa maziwa unaweza kusababisha usumbufu na kuleta maambukizi.

Taulo za matiti (breast pads) ni vitambaa maalum vinavyovaliwa ndani ya sidiria ili kunyonya maziwa yanayovuja kutoka kwenye matiti ya mama anayenyonyesha ambapo zina uwezo wa kufyonza unyevunyevu na kusaidia kuifanya ngozi kuwa kavu na safi na hata pia kuzuia maambukizi ya mama na mtoto wakati wa kunyonyesha.