Na Esther Macha, Timesmajirainline Mbeya
MKURUGRNZI na Mmiliki wa Shule za Sekondari za Patrick Mission na Paradas Mission na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC) Ndele Mwaselela, amesema Rais Samia Suluhu Hassan, anajivunia vijana kwa kuwa ni mboni ya Taifa kwa kulituliza Taifa lao la kesho.
Mwaselela amesema kufuatia ukimnya na amani iliyopo kwa Taifa la Tanzania, kumesaidia Ilani ya CCM kuendelea kutekelezwa kwa vitendo, huku vijana wasomi wa vyuo vikuu wakiwa wanaendelea kusoma wakiwa na utulivu na amani.
Mwaselela amesema hayo mwishoni mwa wiki wakati akizungumza na vijana zaidi ya 400 kutoka makundi mbalimbali katika Mji Mdogo wa Mbalizi katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya.
Hata hivyo, Mwaselela amesema Rais Dkt.Samia ameendelea kuwataka vijana kuendelea kuhuburi umoja na mshikamano na kuwa wamoja bila kujali itikadi na dini zao wala kabila.
Amefafanua kuwa Rais Samia ni mpenzi wa maendeleo ya vijana na watu wazima, wafanyabiashara, wakulima na anajua Taifa zuri litatengenezwa na wasomi kwa haraka.
Akielezea zaidi Mwaselela amesema Rais Dkt.Samia amejipambanua kuwa popote wanapokutana na makundi ya vijana anawahimiza usalama, ulinzi wa Taifa.
More Stories
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu