Na Esther Macha, Timesmajira Online, Mbeya
MKURUGRNZI na mmiliki wa Shule za Sekondari za Patrick Mission na Paradas Mission ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC) Ndele Mwaselela amesema kuwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan anajivunia vijana kuwa mboni ya Taifa ambao wanajielewa kwa kulituliza Taifa lao la kesho ambalo lipo kimya na Kazi zinaendelea kufanyika kwa amani na utulivu.
Mwaselela amesema kuwa kufuatia ukimnya na amani iliyopo kwa Taifa na ilani kuendelea kutekelezwa kwa vitendo huku vijana wasomi wa vyuo vikuu wakiwa wanaendelea kusoma wakiwa na utulivu na amani.
Mwaselela amesema hayo Mei ,26 2024 wakati akizungumza na vijana zaidi ya 400 kutoka makundi mbalimbali katika Mji Mdogo wa Mbalizi katika Halmashauri ya wilaya ya Mbeya wakati wa chakula cha jioni kilicho andaliwa na kiongozi huyo kwenye ukumbi wa Tughimbe.
Hata hivyo Mwaselela amesema kuwa Rais Dkt.Samia ameendelea kuwataka vijana kuendelea kuhuburi umoja na mshikamano na kuwa wamoja bila kujali itikadi na dini zao na kusema kuwa maandiko ya Katiba yetu yanasema CCM itaendelea kuwaunganisha watu usiku na mchana.
“Ndugu zangu vijana Rais Dkt .Samia anasema suala la bumu ni endelevu kichwani mwake na ataendelea kutafakari zaidi na mlimwita kipindi pale mkaenda vijana wote wa vyuo vikuu pale Ikulu mkiomba kuongezewa bumu kutoka sh 8,500 na mkaongezwa ambapo hivi mnapata sh 10,000 lakini pia Rais Samia amenambia endeleeni kusoma na ufadhili wa masomo wa nje ya nchi utaendelea kutolewa”amesema Ndele Mwaselela.
Hata hivyo Mwaselela amefafanua Rais Samia ni mpenzi wa maendeleo ya vijana na watu wazima,wafanyabiashara,wakulima na anajua Taifa zuri litatengenezwa na wasomi kwa haraka na kujali wasomia na hivyo ni lazima kujali makundi ya vijana wote ndi sababu kuu ya kukutana leo .
Akielezea zaidi Mwaselela amesema Rais Dkt.Samia amewaeleza kuwa popote wanapokutana na makundi ya vijana wawahakikishie usalama, ulinzi na Taifa wanalolipenda lina fursa nyingi ambazo wasomi watazipokea na mazingira mazuri yaliyotengenezwa ambayo yatakuwa na uchumi mzuri wa sasa.
Aidha amesema Rais Samia pia ameweza kuboresha mikopo ambapo ameanza ngazi ya Diploma na mikopo ya vyuo vikuu imeongezwa ni kwasababu wapo watoto wa maskini ambao leo hii wangeambiwa kuchangia pesa wengi wangeacha shule ndo sababu mikopo imeongezwa na asimilia kubwa sasa wanapata mikopo bila usumbufu.
“Hata nyie mashaidi wakati Rais Dkt.Samia anaingia madarakani March 19,2021 watu wengi walilalamikia kuhusu bodi ya mikopo leo hii hawalalamiki sababu Rais Dkt.Samia ambaye anadhamila njema na nia dhabiti ya kuhakikisha kuwa mtoto wa mnyonge mtanzania ,Mkulima, mfanyakazi wa chini , mtoto wa Mama Ntilie wote wanakula keki ya Taifa na kufurahia “amesema Mwaselela.
“ Furaha yangu ni kuhakikisha nagusa makundi mbalimbali na kuwa kiongozi ambaye nashuka chini kwenye jami, maana huko ndiko kwenye watu wengi na changamoto lukuki ambazo zinahitaji utashi na upendo wa hali ya juu kwa sisi viongozi tuliopewa dhamani kuzisikiliza, kuzichukua na kuzitatua pale inapobidi”amesena Mwaselela
Kwaupande wao baadhi ya vijana ambao wamejitokeza katika hafla hiyo ya chakula cha jioni ukumbi wa Tughimbe ulipo mji mdogo wa Mbalizi, wamemshukuru MNEC Ndele Mwaselela kwa moyo huo wa pekee, wa kukubali kushuka kwa watu wa chini na kuonyesha upendo wa aina yake bila kujali itikadi za vyama vyao.
Kupitia tukio hilo vijana pia wamepata nafasi ya kuwasilisha changamoto mbalimbali zinazowakabili sehemu za kazi zao, huku wakitoa shukurani kwa serikali kwa kuendelea kutekeleza miradi kadhaa ya maendeleo ndani ya mkoa wa Mbeya na taifa kwa ujumla.
Aidha Mwaselela ameahindi kutoa mikopo kwa mama ntilie 100, pamoja kudhamini mashindano ya mpira wa miguu kwa vijana wa Mbeya Vijijini kwa kata zote kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni thelathini (30,000,000)
Mjumbe wa halmashauri kuu CCM mkoa wa Mbeya,Kenny Laulesi amesema kuwa kitendo kilichofanya na MNEC Mwaselela kukutanisha vijana pamoja ni cha kipekee ambacho lengo kuu ni kufahamu changamoto zao na kuzitatua au kufikisha sehemu husika.
More Stories
TASHICO,yatoa ufafanuzi Mv.Serengeti kutitia upande mmoja
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua