Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
MADIWANI wa wilaya ya Ilala wametakiwa kuacha kupanga safu za Wenyeviti wa Serikali za mitaa au kijiji wasiangaike CCM inataka kuona Mwenyekiti wa Mtaa awe daraja.
Hayo yalisemwa na Katibu wa NEC Idara ya Organizisgeni, Issa Gavu, wakati Mbunge wa jimbo la Ilala Mussa Zungu ambaye ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipokuwa akiwasilisha utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi .
“Nawapongeza Madiwani wa Ilala kwa kujitoa kwenu na kuhakikisha CCM inashika dola ,madiwani wa Ilala wameibeba Tanzania katika Taswira mkoa wa Dar es salaam nawaomba madiwani msipange safu katika uongozi wa Serikali za mitaa Mwenyekiti wa Serikali za mitaa anajiuza kutokana na jitihada zake za utendaji kazi “alisema MNEC Issa .
MNEC Issa Gavu alisema chama cha Mapinduzi CCM inataka kiongozi anayekubalika na jamii sio kushindwa kujiuza marufuku kubeba kiongozi kwa urafiki kupewa madaraka ccm inataka kuona Wenyeviti wa Serikali za mitaa wanafanya mikutano na kuelezea Mapato na matumizi Wenyeviti wa mitaa watakaoshindwa kuelezea Ilani na Mapato ya matumizi wasirudishwe badala yake warudishwe wachapakazi
Alisema katika chaguzi za Serikali za mitaa ukichagua kiongozi boya adhabu yake miaka mitano kwani kiongozi mzuri ana faida ndani ya chama na Jamii anayoongoza.
MNEC Issa alisema chama kwanza mtu baadae viongozi wa Serikali za Mitaa wasiojituma na kufanya kazi wametakiwa kuajibika na kurudi katika mstari Mwenyekiti wa mtaa asiyefanya kazi atoshi kushika dola
Aliwataka wilaya ya Ilala wajipange katika kuboresha Daftari la wapiga kura kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka 2024 na uchaguzi Mkuu 2025 mpiga kura lazima usajiliwe katika Daftari hivyo wametakiwa kuwahamasisha wana ccm kwa wingi katika Daftari hilo hivi karibuni.
Akizungumzia mafanikio ya Jimbo la Ilala na utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi uliofanywa na Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu ,alisema Ilala sasa hivi wanatembea kifua mbele hivyo aliwataka wabaki katika umoja na kujenga mshikamano kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan amefanya makubwa kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo sekta ya afya ,sekta ya Elimu miundombinu ya Barabara
Alisema mkutano huo wa jimbo la Ilala ni shamba darasa kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za mitaa 2024 na uchaguzi mkuu 2025.
Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu katika mkutano huo wa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani pia aliwapa mafunzo yaliondanguliwa na semina ya Shirika la Umeme Tanamza TANESCO kwa wajumbe wote wa mkutano wa jimbo la Ilala ambapo viongozi hao wa chama wamelijua vizuri Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)ili wakaeleze kwa wananchi katika kuisaidia Serikali.
Mbunge zungu alisema amechaguliwa mwaka 2020 kila mwaka anawasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya chama kwa vile wanasimamia Ilani ya chama umati huo wa mkutano mkuu wa jimbo ndio jeshi la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan .
Alisema kuna mambo mengi yanafanywa Serikali katika utekelezaji wa Ilani lakini wananchi hawayaoni amewataka wananchi
kumpa ushirikiano ili kuleta maendeleo jimbo la Ilala.
Alisema TANESCO inaongoza mapato mengi Tanzania kutoka Ilala watumiaji nishati hiyo wengi.
Alisema katika jimbo hilo mvua zitakapomalizika barabara zote za kisasa zitajengwa kwa kiwango cha lami hivyo aliwataka wananchi kuwa na subira na uvumilivu.
Mbunge Mussa Zungu alitumia fursa hiyo kumpoza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa pesa nyingi za miradi ya maendeleo ikiwemo sekta ya afya, sekta ya Elimu na miundombinu ya Barabara.
More Stories
TASHICO,yatoa ufafanuzi Mv.Serengeti kutitia upande mmoja
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua