Na David John Geita
WAZIRI wa Madini Antony Mavunde amesema serikali itaendelea kusimamia sheria ya wawekezaji wazawa ili kuhakikisha watanzania wananufaika na rasilimali zao ikiwemo madini yanayochimbwa katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Aidha Waziri huyo amewaasa wawekezaji wengine kichangamkia fursa hiyo ya kufanya uwekezaji mkubwa hapa nchini kwa.maslahi Yao na maslahi mapana ya Taifa .
Akizungumza katika halmashauri ya mji wa Geita alipotembelea Mwekezaji mzawa Athanas Inyasi wa Kampuni ya Blue Coast,Waziri Mavunde amesema Sheria hiyo ni miongoni mwa mambo yanayowafanya wazawa kufanya uwekezaji wenye tija hapa nchini.
Amewaasa wafanyabiashara ,wachimbaji kujitokeza kuomba zabuni Ili waweze kufanya uwekezaji ambao tayariazingira yake yameshabireshwa na Rais Samia Suluhu Hassan na hivyo kuwafanya wawekezaji kufanya biashara zenye tija kwa nchi.
Aidha Waziri Mavunde amesema kuwa uwekezaji wa kampuni ya blue cost umesaidia kutoa ajira nyingi kwa vijana wakitanzania pamoja na kuchangia mapato ya halmashauri pamoja na kodi ya Serikali hivyo uwepo wake una maana kubwa katika maendeleo ya nchi na hususani mkoa wa Geita.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Makampuni ya Blue Cost ,Athanas Inyasi amesema uwepo wa sheria ya wawekezaji wazawa l(ocal Contect ) ,imesaidia kwa kiasi kikubwa kutokana na kuleta mafanikio makubwa kwa watanzania,huku ajira 360 zikiwa zimetolewa na kampuni hiyo.
Akitoa taarifa fupi ya Kampuni hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Blue Coast Ndahilo Athanas amesema kampuni hiyo pia katika kurudisha kwanjamii kinachopatikana ,wanajenga miundombinu mbalimbali huku akisema kmaouni imejenga madarasa lakini pia menunua madawati kwa shule za msingi Nyamalembo na Mseto zilizopo mkoani Geita .
Naye Mkuu wa Mkoa wa geita,Martine Shigela ametumia nafasi hiyo kuwataka wachimbaji wadogo pindi wanapopata fedha waweze kubadilisha biashara ambazo zitawaongezea kipato.
Aidha amesema uwepo wa Local Contect umeongeza kwa kiasi kikubwa ajira kwa watanzania na kutoa fursa za wazawa kupata manufaa kutokana na shughuli ambazo zinafanyika kwenye maeneo yao.
More Stories
Gridi za Tanzania, Kenya kuimarisha upatikanaji wa umeme
Mama Zainab:Watoto yatima ni jukumu la jamii yote
DC Korogwe awataka viongozi wa vijiji kuwatumikia wananchi kwa uadilifu