Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
Tanki la Mafuta na gesi
limelipuka Kata ya Kisukuru wilayani Ilala, wakati mafundi wakichomea na kuleta maafa kwa fundi mmoja aliyetambulika kwa jina la Haassn Salehe na fundi mwingine hali yake mbaya .
Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam Jumnne Mulilo, amethibitisha tukio hilo ambapo amesema alipata taarifa ya mlipuko wa Tanki hilo la mafuta ambalo limeleta kizaa zaa kwa nyumba zaidi ya 11 kuvunjika vyoo,milango na Singibord mara baada tanki la mafuta kulipuka katika sehemu ya kuifadhi magari ambayo imejengwa katika makazi ya wananchi.
“Ni kweli jana majira ya saa moja jioni nilipokea taarifa ya mlipuko wa gesi uliolipua tanki la Mafuta Kisukuru Wilaya ya Ilala na kusababisha kifo cha Fundi Hassan Salehe,aliyekuwa akichomelea na kijana mwingine hali yake mbaya bado yupo hospitali wote walipata madhara katika mlipuko wa tanki la mafuta “Kamanda Mulilo.
Kamanda Jumanne Mulilo, alisema madhara mengine yaliotokea katika mlipuko huo wa tanki la mafuta na mtungi wa gesi nyumba zaidi ya 11 zimevunjika vyoo na milango kutokana na mtikisiko wake kuwa mkubwa
Kamanda Mulilo alisema Mmiliki wa sehemu hiyo ya kuifadhi magari anaitwa Juma Jabir ,Kabila lake Msambaa na Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wake kwa sasa .
Diwani wa Kata ya Kisukuru Lucy Lugome ,alisema janga hilo la mlipuko ulitokea jana ambapo umesababisha kifo cha mtu mmoja na nyumba 14 kupata madhara ambapo kwa sasa Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Ilala imeunda tume maalum kwa ajili ya kuchunguza tukio hilo.
Diwani Lucy Lugome aliwataka wakazi wa Kisukuru Magoza kuwa wavumilivu katika janga la ajali hiyo wakisubiri Serikali kumaliza kufanya uchunguzi wake.
Waziri Mstaafu wa Serikali ya awamu ya nne Hamza Abdalah Mwinyigoha, ambaye anaishi eneo la tukio hilo alisema wakati mlipuko unatokea nyumbani kwake wajukuu walikuwa hawapo endapo wangekuwepo maafa yangekuwa makubwa kwani Mara baada mlipuko huo nyumba yake imepata madhara makubwa milango kupasuka na vyoo kuvunjika kwa madirisha .
Hamza Abdalah Mwinyigoha alisema katika nyumba yake athari kubwa imetokea ikiwemo kuharibu Mali na vitu vya thamani.
Alisema ameshangazwa gereji hiyo kubwa kukaa katika makazi ya wananchi hivyo wameomba Serikali iweze kuchukua hatua kwa ajili ya usalama wa wananchi wa eneo hilo la Kisukuru.
Mjumbe wa Shina namba 8 Kisukuru Magoza Frola Mwakanyamale, alisema tukio limetokea jana Agosti 27 nyumba yake inapakana na sehemu ya tukio ambapo anamshukuru Diwani wake Lucy Lugome kwa kuwakimbilia na kutoa msaada wa Haraka.
More Stories
Serikali kupeleka mawasiliano maeneo ya mipakaniÂ
Sekondari ya Butata mbioni kufunguliwa Musoma Vijijini
TIC yapongeza mradi wa Kampuni ya Big Best