Na Mwandishi Wetu, Timesmajira
Tanzania ni miongoni mwa maeneo ya dunia yaliyopendelewa kwa kiasi kikubwa na Mwenyezi Mungu. Kupendelewa huko kunatokana na kuwa miundombinu mingi ya asili ambayo kama yatatumika vizuri yatakuja kuleta faida na maendeleo kwa faida ya Taifa la Tanzania na wananchi wake.
Hayo yamesemwa na mwenyekiti mstaafu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Morogoro Mjini, Salum Mkolwe alipokuwa akifanya mahojiano na mwandishi wa Timesmajira.
Mkole amesema, kwa sasa watanzania wanatakiwa kuacha malumbano katika mambo ambayo yako wazi kuwa uwekezaji wa Bandari nchini, utakuwa na tija katika nyanja mbalimbali.
Amesema, kitu kikubwa ambacho Serikali ya Rais Dkr. Samia Suluhu Hassan imekuwa ikijitahidi ni, kutafuta ajira kwa wananchi wake hasa vijana kwa kufungua sekta ya biashara na kilimo.
Hivyo uwekezaj unaotaka kufanywa na kampuni ya DP Word ya Dubani, katika uendelezaji na uendeshaji wa Bandari unaweza kuleta ajira nyingi hasa kwa vijana.
Hata hivyo amesema, kwa jinsi wanavyoisoma kampuni ya DP Word inauwezo mkubwa wa kuifanya bandari kuwa na uwezo mkubwa wa kuhudumia wafanyabiashara wengi tena kwa muda mfupi.
“DP World ni Kampuni kubwa inayoweza kuhudumia wateja wengi Bandarini kwa muda mfupi, hivyo watanzania hawana haja ya kuogopa tuunge mkono,” amesema Mkolwe.
Mbali na hivyo, pia amesema duniani hakuna mkataba usio na kikomo na kuvunjwa pale unapokiukwa au unapotakiwa kufanyiwa marekebisho, hivyo wasitishwe na wananchi wachache ambao hawana nia njema ya kuhakikisha Tanzania inapiga hatua.
“Nchi yetu ina wanasheria nguli na wenye weledi katika masuala ya mikataba ya uwekezaji baina ya Serikali na Sekta binafsi kutoka nje ya nchi, hivyo wakati wa kusaini mikataba mahususi na kampuni ya DP World ni dhahiri kila jambo litafanyika kwa mujibu wa sheria na kuweka maangalizo ambayo hayana madhara kwa Taifa,” amesema.
Kada huyo ana amini hayo yote yanatokana na uongozi bora wa Rais Dkt. Samia kwa kuweka mikakati ya kuinua uchumi na kipato kwa mwananchi mmoja mmoja.
Pamoja na hayo Uwekezaji huo utaifanya Bandari kuwa lango kuu la uchumi wa mataifa ya DRC, Rwanda, Burundi, Zambia, Uganda na Malawi ambapo uletaji wao mizigo utakuwa na manufaa kwa taifa katika suala zima la kuongeza mapato.
Amemuomba Rais Dkt. Samia kuendelea kuweka mazingira wezeshi ili kuvutia wawekezaji wengi zaidi wa ndani na nje ya nchi katika Sekta mbalimbali ili kuendelea kupata mapato yatokanayo na uwekezaji na hatimaye faida itakayopatikana, iweze kuchangia kwenye bajeti kuu ya Serikali na hatimaye kuwa chachu ya maendeleo kwa Taifa.
More Stories
Kamishna Hifadhi ya Ngorongoro atakiwa kupanua wigo wa Utalii nchini
Wakuu wa Wilaya,Wakurugenzi watakiwa kusimamia programu za chakula shuleni
Mbowe akuna wengi kuhusu maridhiano