November 14, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mkojo wa Sungura watumika kufukuza wadudu katika mbogamboga na matunda


Na Penina Malundo,timesmajira, Online


KUTOKANA  na mfumo wa ulaji kubadilika na watu kupenda kula Chakula cha asili,Chuo Kikuu Mzumbe kimekuja na  ubunifu wa mkojo wa Sungura kwa kilimo Cha matunda na mbogamboga.
Katika kufanya tafiti zake,Chuo kimegundua kuwa mkojo wa Sungura unaharufu kali hivyo  sio rafiki kwa wadudu hasa wale waharibifu katika  mboga zenye jamii ya maua na matunda.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika maonesho ya 46 ya Kimataifa ya biashara yanayofanyika katika Viwanja vya Sabasaba,Mwanafunzi wa Sayansi ya Uzamili Chuo Kikuu cha Mzumbe, Nelson Kissanga amesema kuja na mfumo huo kwa wakulima wameunga mkono kauli ya  Rais Samia Suluhu Hassan  kuwa Tanzania ni mahali sahihi ya Biashara na Uwekezaji.
Amesema   Chuo chao pia  kinandaa wataalamu kwa kauli mbiu ya kujifunza kwa maendeleo ya watu.”Tumekuja na ubunifu huu ambao utasaidia wakulima kutopata hasara pindi wadudu watakapoingia katika bustani na kuharibu mbogamboga na matunda,”amesema na kuongeza 
” wadudu  ni waharibifu katika mbogamboga na mboga zenye jamii ya maua pamoja na matunda kwani  wanapenda kuvutiwa sana na mvuto wake katika kufata harufu nzuri ya maua hasa yanapochanua,”amesema Kissanga
Amesema Mkojo wa sungura ni mbadala wa utumiaji wa kupuliza madawa katika mbogamboga na matunda ambapo yanakuwa na madhara kwa watu wengi.

“Mkojo huo wa sungura ni  fursa  kwa watu wengi kwani unapowafuga sungura na kupata mkojo wao,mfugaji anapaswa kujenga banda la juu (gorofa)kidogo hivyo wanapokojoa kunakuwa na kinga zinazokuwa zinakinga mkojo wao,”amesema Kissanga
Aidha amesema mkojo huo   hauna shida yoyote  kwa watumiaji kwani hauna kemikali yoyote, unakuwa ni mkojo halisi unaotoka kwa Sungura .
Amesema hii itawasaidia  watu kubadilika kutumia vyakula venue kemikali na kula    vitu vya asili kwani gharama za kemikali katika kununua zinakuwa juu kuliko mkojo wa sungura. 
“Tumeongeza mnyororo wa thamani wa  mfumo huu wa mkojo wa  sungura ni rafiki wa mazingira na rahisi kutumia tunaomba watu wawe tayari kuupokea na kuutumia waone kama fursa,”amesisitiza
Kwa upande wake,Mwanafunzi wa Chuo cha Mzumbe Maziku Maziku, amesema wamebuni teknolojia ya Unikopa katika kusaidia wanafunzi kukopa  mkopo wa simu,fedha na laptop.
Amesema unikopa katika vyuo vikuu imekuja  baaada ya mikopo kuonekana wanafunzi wanakuwa na changamoto mbalimbali katika kupata mitaji.
“Wanafunzi wengi wanakutana na changamoto ya kupata fedha kwa urahisi zaidi kwani wanakopeshwa hawana dhamana ya  nyumba na fedha kwahiyo mfumo huu ni rahisi kwao kwani hauna riba yoyote,”amesema
Amesema mpaka sasa wanawanafunzi 1320 ambao wamejisajili  katika  mfumo huo  kutoka chuo kikuubchabDar es Salaam, Mzumbe ,Ardhi  na Udom .