Na Judith Ferdinand, TimesMajira Online, Mwanza
Mkoa wa Mwanza umevuka lengo katika zoezi la utoaji wa chanjo ya polio kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano kwa kufanikiwa kuwachanja jumla ya watoto 965,229.
Huku Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba ikiongoza katika zoezi kwa kuwachanja watoto wengi ambapo jumla ya 138,758 lengo lilikuwa kuwachanja watoto 134,636 huku Nyamagana ikiongoza kwa asilimia ambapo imefikia asilimia 125 ya malengo iliojiwekea.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel, katika kikao cha kupitia utekelezaji wa mkataba wa lishe,kupata taarifa ya kampeni ya chanjo ya polio na maandalizi ya kampeni ya chanjo ya uviko-19 kilichofanyika jijini Mwanza.
Mnamo tarehe 18 hadi 21 Mei, 2022 kulifanyika kampeni ya utoaji chanjo ya matone ya kuzuia ugonjwa wa polio, ikiwa ni moja ya mikakati ya kuzuia ugonjwa huo usiingine hapa nchini mara baada ya nchi jirani ya Malawi kutokea kwa mlipuko,
Ambayo ilihusisha kuchanja watoto wote wenye umri chini ya miaka mitano bila kujali chanjo ambazo alizipata kabla ya kampeni.
“Mkoa wetu ni miongoni mwa mikoa nchini ambayo ilifanya vizuri kwa kufanikiwa kuchanja jumla ya watoto 965,229 kati ya watoto 846,773 waliotarajiwa kuchanjwa,halmashauri zote zilifanya vizuri kwa kuchanja watoto zaidi ya lengo lililokuwa limewekwa,ili kuhakikisha nchi yetu inakuwa salama juu ya hatari ya ugonjwa wa polio, bado tunatakiwa kuendelea kutoa chanjo hiyo kwenye vituo vyote vya huduma za afya,”ameeleza Mhandisi Gabriel.
Pia ameeleza,kuwa kila mtoto anayezaliwa na ambaye hajapata chanjo hiyo, anatakiwa apate angalau dozi mara nne tangu kuzaliwa kwake na kabla hajakamilisha umri wa mwaka mmoja huku chanjo ya nyongeza hutolewa kwenye kampeni maalumu kama ilivyofanyika mwezi Mei mwaka huu.
Hivyo, kuna awamu nyingine zitafuata kati ya mwezi Julai na Agosti mwaka huu ikiwa ni mikakati ya kuhakikisha kirusi cha ugonjwa wa Polio hakiingii nchini hapa.
Kwa upande wake Mratibu wa Chanjo Mkoa wa Mwanza Amos Kiteleja,akiwasilisha taarifa ya ufanisi wa zoezi hilo la chanjo katika kikao hicho,ameeleza kuwa Halmashauri zote za Mkoa huo zimefanya vizuri na kuvuka lengo.
Ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba ikiongoza kuchanja idadi kubwa ya watoto 138,758 huku lengo likiwa 134,636 ikifuatiwa na Misungwi ambao wanechanja watoto 127,101 wakati malengo ilikuwa ni kuchanja watoto 116,207.
Halmashauri ya Buchosa ikishika nafasi ya tatu kwa kuchanja watoto 124,143 huku malengo yalikuwa ni kuwafikia watoto 106,143 ikifuatiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe ambayo walilenga kuchanja watoto 108,937 lakini walifanikiwa kuchanja watoto 122,259.
Ambapo Halmashauri ya Wilaya ya a Sengerema ambayo lengo lilikuwa kuchanja watoto 108,937 huku walifanikiwa kuchanja watoto 119,279 huku Wilaya ya Nyamagana ikifanikiwa kuchanja watoto 116,334 huku lengo lilikuwa ni kuchanja watoto 92,698.
Huku Halmashauri ya Wilayani ya Magu ikichanja watoto 109,119 uku lengo likiwa ni kuwafikia watoto 93,721 huku Wilaya ya Ilemela ikifanikiwa kuchanja watoto 108,236 ambapo malengo yao yalikuwa ni kuchanja watoto 85,834.
Kiteleja ameeleza kuwa, miongoni mwa changamoto zilizojitokeza katika zoezi hilo ni pamoja na baadhi ya familia kukataa watoto wao wasichanjwe wakihusisha chanjo hiyo na chanjo ya uviko-19.
“Halmashauri ya Misungwi Mganga Mkuu alichukua jukumu la kutembelea familia zilizokataa kuchanjwa na kuwaelimisha wakakubali kuchanjwa na jumla ya watoto 11 walipata chanjo hiyo,” ameeleza Kiteleja.
Naye Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza Dkt.Sebastian Pima,ameeleza kuwa wameongoza katika zoezi hilo kwa upande wa asilimia kutokana na ushirikiano.
“Katika zoezi hilo tumeweza kufanya vizuri kwa kufikia asimilia 125 ya malengo kwa sababu,tuweza kufikia jamii kupitia viongozi wetu wa mitaa ambao wakitusaidia katika kampeni yetu ya nyumba kwa nyumba kwa asilimia 100,tuliwahusisha watoa huduma ya afya ngazi ya jamii ambapo malengo ilikuwa ni kufikia watoto 92,698 na tumeenda zaidi hadi kufikia watoto 116,334,”ameeleza Dkt.Pima.
More Stories
ITA chatakiwa kutoa mafunzo ya viwango vya juu na kasi ya maendeleo ya Kisayansi
Wagombea CHADEMA wakipewa ridhaa,watakuwa wawazi
TTCL yafanya maboresho katika huduma zake