Na Iddy Lugendo, Timesmajira Online
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf amesema serikali inazingatia suala la Usalama na Ulinzi wa watoto katika Taasisi za Elimu na Vyuo n kuhakikisha hakuna unyanyasaji wa kijinsia.
Prof. Mkenda ametoa kauli hiyo Julai 22, 2023 wakati akizindua Mwongozo wa Ulinzi na Usalama wa Wanawake na Vijana katika Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi (FDCs), Vyuo vya Ualimu na Vyuo vya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA).
Uzinduzi wa Mwongozo huo umefanyika katika Chuo cha Maendeleo ya Wananchi (FDC) Mto wa Mbu Wilaya ya Monduli mkoani Arusha ukiongozwa na kauli mbiu inayosema ” ULINZI VYUONI UNAIMARISHA UTOAJI ELIMU BORA, YENYE USAWA KWA MAENDELEO ENDELEVU TANZANIA”*
Amesema usalama wa wanafunzi ni suala muhimu sana kwani wanafunzi Wazazi wanapeleka waoto vyuoni wana kuwa na imani juu ya usalama wao.
Mkenda amesema Mwongozo uliozinduliwa unezingatia mahitaji na hivyo unakwenda kuchochea kuongeza umakini katika kuwalinda wanafunzi wote na jamii inayozunguka vyuo dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji wa aina zote ili mwisho wa siku wapate elimu na ujuxk kuwawezesha kushiriki katika shughuli za kiuchumi.
Prof. Mkenda ameishukuru serikali ya Canada kwa kutoa ufadhili wa Dola milioni 25 za Canada zitakazotumika kutoa Elimu kwa Wasichana ili kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika mafunzo na shughuli za Kiuchumi.
Awali akizungumza kuhusu utekelezaji wa Mradi wa Uwezeshaji Kupitia Ujuzi (ESP) Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kimataifa Jumuiya na Taasisi za Vyuo Canada (CiCan) Caroline Marrs amesema miongoni mwa kazi zinazotekelezwa na Tasisi hiyo ni pamoja na Kujenga uwezo wa kuunda Mitaala ili kutoa Mafunzo yenye Ujuzi ndani yake, dhana inayofahamika kama Elimu kwa Ajira.
Nae Rais na Mkurugenzi Mkuu wa Jumuiya na Taasisi ya Vyuo Canada (CiCan) Denise Amyot amebainisha kwamba, katika Mradi huo wa ESP wanazingatia sana suala la Uwezeshaji wa Kiuchumi kwa Wanawake na Wasichana ili kwenda sambamba na lengo namba Tano la Maendeleo Endelevu linalohusu usawa wa kijinsia
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba