November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mkenda azindua Bodi ya TCU

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma

WAZIRI  wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda ameitaka Bodi ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) ifanye kazi kwa kuzingatia kanuni ,sheria na taratibu ili waweze kutenda haki katika utekelezaji wa majukumu yao.

Waziri Mkenda ameyasema hay oleo Januari 19,2023 jijini Dodoma wakatika akizundua Bodi mpya ya Tume ya Vyuo Vikuu baada ya Bodi iliyopita kumaliza muda wake.

“Mna kazi  kubwa ya kuwezesha na kudhibiti hivyo tumieni nafasi hiyo kuifungua nchi katika sekta ya Elimu,msimuonee mtu wala msikubali kutumika kwa namna yoyote ile,mnachopaswa ni kufuata sheria,taratibu na kanuni zinazowaongoza.”amesema Profesa Mkenda na kuongeza kuwa

“Kazi yenu ina lawama sana hasa pale mnapotaka kutekeleza jukumu la kudhibiti hapo lazima mguse watu hivyo msiogope kwani kufanya hivyo itasaidia kuongeza ubora katika sekta yetu ya Elimu hasa Elimu ya vyuo vikuu ambayo ndio muhimili wa Taifa letu,” Amesisitiza Mkenda

Waziri Mkenda pia ameitaka Bodi hiyo ya TCU kuhakikisha wanawezesha vyuo kufanya udahili na kuhakikisha elimu inayotolewa Vyuoni iwe bora na Ufaulu uwe mzuri ili kutengeneza taifa lenye watu wasomi wanaokidhi vigezo.

Aidha, Prof.Mkenda ameitaka Bodi hiyo kuwezesha utambuzi wa vyuo vikuu vya nje ya nchi ikiwezekana kwenda kufanya uchunguzi kuhusu ubora na nafasi ya vyuo hivyo katika nchi zao ili kuwasaidia vijana wa kitanzania wanapokwenda kusoma nje wasome katika vyuo bora na vyenye ushindani.

“Jaribuni kutambua vyuo vinavyofundisha wanafunzi wetu huko nje na mjaribu pia kufanya tafsiri ya elimu inayotolewa katika vyuo hivyo ili kuwawezesha wanafunzi wetu wanaomaliza huko nje na kurudi nyumbani waajirike tusiishie tu kuwapeleka alafu kwenye soko la ajira hatuwaoni,”amesema Profesa Mkenda

Naye Profesa Penina Mlama amemhakikishia Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe.Prof Adolf Mkenda kuwa watatekeleza maelekezo yote aliyowaagiza iliwemo kuifungua nchi kimataifa kwa kuwapeleka wanafunzi wengi kusoma Vyuo vya nje ya nchi,Kuongezeka kwa kasi ya Udahil,kusimamia ubora wa elimu inayotolewa na kuhakikisha vyuo vikuu vinasimama imara kuhimili na kuyamudu mabadiliko yanayotokea duniani.